Tanzania, Kenya zazindua mkongo wa mawasiliano

SERIKALI  za Tanzania na Kenya zitaimarisha diplomasia ya kidijitali na biashara baada ya kuzindua mkongo wa mawasiliano baina ya nchi hizo.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Mawasiliano na teknolojia yaHabari Jerry Silaa ,wakati wa uzinduzi wa maunganisho ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB) wa TTCL  na mikongo ya bahari iliyopo Mombasa kupitia ICTA Kenya katika eneo la Horohoro wilayani Mkinga mkoani Tanga.

Amesema kuwa kupitia mkongo huo, wananchi wataweza kupata huduma nafuu ya mtandao kutokana na kuimarika kwa miundombinu hiyo.

“Tunakwenda kuangalia sera zetu katika maeneo ya kutolea huduma baina ya nchi zetu, ili wananchi waweze kupata huduma bora za mawasiliano,” amesema Waziri Silaa.

Naye Waziri wa Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Kidijitali wa Kenya, William Gitau amesema kuwa mkongo huo utaimarisha ubunifu wa kiteknolojia kwa wananchi wa nchi hiyo

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button