Tanzania, Kyrgyzstan kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mahmoud Thabit Kombo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kyrgyzstan, Zheenbek Kulubaev, wamesaini Tamko la Pamoja kuanzisha Uhusiano wa Kidiplomasia baina ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Kiyrgystan.

Tamko hilo limesainiwa Septemba 26, 2025 katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Pamoja na tamko hilo, uhusiano wa kidiplomasia baina ya nchi hizi mbili utaongozwa na mkataba wa Vienna unaosimamia Uhusiano wa Kidiplomasia (Vienna Convention on Diplomatic Relations, 1961) na sheria nyingine za kimatiafa.

Waziri Kombo aliipongeza Kyrgyzstan kwa uamuzi wake wa kufungua ubalozi jijini Addis Ababa, akisema kuwa hatua hiyo ya kimkakati itarahisisha mawasiliano ya moja kwa moja na nchi za Afrika na itaimarisha ushirikiano na Tanzania kupitia Ubalozi wake nchini Ethiopia ambapo Balozi wake pia ni Mratibu Mkuu wa Masuala ya Umoja wa Afrika, nchini humo.

Aidha, alibainisha kuwa maendeleo makubwa ya Kyrgyzstan katika sekta ya elimu yameifanya sekta hiyo kuwa lango muhimu la ushirikiano, ambapo alipendekeza nchi hizo kuanzisha jukwaa la mazungumzo ya kiuchumi au kisiasa, litakalowakutanisha wataalam kutoka pande zote mbili na kujadili namna bora ya kuanzisha ushirikiano katika maeno mbalimbali ya kisekta na hivyo kuleta maendeleo endelevu kwa wananchi wake.

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Kyrgyzstan, Kulubaev alieleza ni yao ya kuanza kujifunza lugha za Afrika kama vile Kiswahili kwa urahisi wa kufanya mazungumzo na Afrika ikiwemo Tanzania.

Kuhusu laugha za kiafrika na Kiswahili, Waziri Kombo alieleza imani yake ya kuwa Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dk. Salim Ahmed Salim cha Dar es Salaam kina uwezo wa kuhakikisha azma hii inatekelezwa kwa manufaa ya pande zote.

Hatua hiyo itakiwezesha kituo hicho kuwa jukwaa la mafunzo na ubadilishanaji wa uzoefu, jambo ambalo litasaidia kuimarisha uhusiano ya kidiplomasia na kukuza mawasiliano ya kiutamaduni baina ya Tanzania na Kyrgyzstan, alisisitiza Waziri Kombo.

Waziri Kulubaev alitumia mazungumza hayo, kuisihi Serikali ya Tanzania kuwashawishi wanafunzi wa Tanzania kujiunga na vyuo vikuu vya Kyrgyzstan, hasa kwenye programu za udaktari ambazo tayari zimevutia wanafunzi wengi kutoka nchi za Bangladesh, Pakistan na India.

“Serikali ya Kyrgyzstan iko tayari kuwasilisha kwa Tanzania taarifa kuhusu programu, ada na gharama za maisha ili kusaidia wanafunzi kupanga masomo yao na wafadhili wao kutambua gharama husika za kufadhili”, alifafanua Mhe. Waziri Kulubaev.

Mhe. Kulubaev ameisihi Serikali ya Tanzania kurahisisha upatikanaji wa viza kwa raia wa Kyrgyzstan wenye pasipoti za kidiplomasia na za utumishi, na hatimaye kwa wale wenye pasipoti za kawaida, ili kurahisha usafiri wa watu na bidhaa na ikiwa na sehemu ya kuimarisha husiano ya kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button