Tanzania, Marekani kushirikiana kibiashara

DAR ES SALAAM: SERIKALI ya Tanzania na Marekani zimeingia makubaliano ya majadiliano ya kibiashara yatakayosaidia upatikanaji wa masoko ya bidhaa.

Makubaliano hayo yameingiwa leo Oktoba 19, 2023 jijini Dar es Salaam, mbele ya Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Ashatu Kijaji ambaye amesema jitihada kubwa zinahatajika kukuza biashara na uwekezaji kwenye vipengele mbalimbali ikiwemo uchumi wa kidijitali na upatikanaji wa masoko nchini Marekani.

Kijaji amesema hati hiyo ya makubaliano ya majadiliano itasaidia kukuza biashara ya Tanzania na uendelezaji wa biashara kati ya Tanzania na Marekani ili kukuza uchumi.

Aidha, Dk Kijaji amesema biashara ya Tanzania kwa marekani bado ni ndogo sana, haijakidhi fursa zilizopo nchini hadi kufikia mwaka 2022, mauzo ya Tanzania kwenda Marekani yalikuwa ni Dola milioni 74.5 pekee.

Naye, Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Michael Battle amesema uhusiano wa Tanzania na Marekani una nguvu sana katika maendeleo ya kiuchumi

Kwa upande wa Mkurugenzi wa shirikisho la wenye viwanda Tanzania Leodgar Tenga amesema wanafurahia sana kuwa na uhusiano nzuri

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button