Tanzania mwenyeji mkutano wa kahawa Afrika

DAR ES SALAAM: MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amesema nchi 25 za Afrika zitahudhuria mkutano wa tatu wa nchi zinazozalisha kahawa utakaofanyika nchini kuanzia Februari 21-22, 2025 wenye lengo la kukuza na kujadili zao hilo.

Mkutano utaudhuriwa na mawaziri wa kilimo wa nchi hizo na wakuu wa nchi hizo huku zaidi ya washiriki zaidi ya 1,000 kutoka ndani na nje ya nchi.

Chalamila amesema mkutano huo ni wa tatu kufanyika hapa nchini hivyo una tija kwa taifa hivyo wafanyabiashara wa zao hilo wajitokeze kunadi zao hilo ili wawe na manufaa nalo wao binafsi na nchi kwa ujumla.

SOMA ZAIDI: Tanzania mwenyeji kongamano utalii wa vyakula Afrika

“Viongozi wa wakuu wa nchi wanategemewa kuwa sehemu ya huu mkutano ambao kwa tarehe 21 ni kwa mawaziri wa kilimo kutoka nchi zote na tarehe 22 ni kwa wakuu wa nchi kutoka nchi hizo wale ambao wanaweza kuwa wamethibitisha mkutano huu ni muhimu sana kuzungumzia mkutano huu hususani kwa jiji la Dar es Salaam,” amesema Chalamila.

Chalamila amesema kuhusu kufungwa kwa barabara hazitofungwa bali barabara itakayotumika kwa wageni ni barabara inayotoka kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere kuja mjini hivyo hakutakuwa na magari, pikipiki na bajaji zitakazopita barabara hiyo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button