Tanzania, EU waimarisha ushirikiano kibiashara

DAR ES SALAAM: Tanzania na Umoja wa Ulaya wameendelea kuimarisha ushirikiano katika biashara, uwekezaji, maendeleo ya miundombinu pamoja na kukuza sekta binafsi kwa kipindi cha miongo mitano iliyopita.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga Mei 07, 2026 jijini Dar es Salaam, na kubainisha kuwa Umoja wa Ulaya umeendelea kushirikiana na Tanzania katika maeneo muhimu ikiwemo maendeleo ya rasilimali watu, uchumi wa kijani, mageuzi ya kidijitali, uchumi wa buluu pamoja na maendeleo ya biashara na viwanda.

Amesema kupitia programu za Global Gateway na Team Europe, Tanzania imeendelea kunufaika na uwekezaji katika nishati, mifumo ya kidijitali, bandari na miundombinu ya usafiri, hali iliyoongeza fursa za biashara na ushindani wa kiuchumi.

Waziri Kapinga amesema ushirikiano huo pia umeendelea kufungua masoko, kuimarisha minyororo ya thamani na kuongeza fursa kwa biashara ndogo na za kati (SMEs), hatua inayochochea ajira na ukuaji wa uchumi wa ndani.

Aidha, amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Umoja wa Ulaya katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ili kuhakikisha wananchi na sekta binafsi wanaendelea kunufaika na matokeo ya ushirikiano huo.





I tried a similar approach with rosemary last week, but the flavor was a bit too strong for my liking. Maybe a lighter hand is needed next time, or a different herb entirely. What do you think about marjoram as a substitute here?