Tanzania, Uturuki kuimarisha biashara

SERIKALI imesema inataka kuongeza kiwango cha mauzo ya bidhaa nchini Uturuki.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Selemani Jafo alisema hayo Dar es Salaam jana wakati wa kusaini Azimio la Kamati ya Pamoja ya Biashara (JTC) kati ya Tanzania na nchi hiyo.

Dk Jafo alisema ushirikiano huo unalenga kuongeza mauzo ya bidhaa za Tanzania nchini Uturuki na kujenga uchumi imara kupitia diplomasia ya uchumi.

“Kupitia timu ya wataalamu na ushirikishwaji wa sekta binafsi, tutashirikiana katika biashara kama lango kuu la fursa. Lengo kuu la viongozi wetu ni kuongeza mauzo,” alisema.

Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2024 kiwango cha biashara kati ya nchi hizo mbili kilifikia Dola za Marekani milioni 284, huku mauzo ya Uturuki kwenda Tanzania yakifikia Dola za Marekani milioni 217.

“Tunafahamu wenzetu wa Uturuki wameendelea sana upande wa teknolojia, hasa katika sekta ya kilimo na viwanda. Ushirikiano huu utawawezesha Watanzania kupata tija upande wa uwekezaji na kuchangia maendeleo ya nchi yetu,” alisema Dk Jafo.

Alisema uhusiano kati ya Tanzania na Uturuki umeimarika hasa tangu kufunguliwa tena kwa Ubalozi wa Uturuki nchini Tanzania mwaka 2009 na kuanzishwa kwa Ubalozi wa Tanzania Uturuki mwaka 2017.

Dk Jafo alisema ziara za viongozi wakuu ikiwemo ya Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdoğan nchini Tanzania na ziara ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan nchini Uturuki mwaka 2024 zimeimarisha zaidi ushirikiano huo.

Alisema kampuni za Kituruki zimekuwa washirika katika miradi mikubwa ya maendeleo ukiwemo ujenzi wa reli ya kisasa (SGR).

“Makampuni ya Uturuki hasa kwenye SGR yameweza kufanya biashara ambayo italeta fursa nyingi kwa wananchi wetu hasa kwenye eneo la ajira,” alieleza Dk Jafo.

Naye Kaimu Balozi wa Uturuki nchini, Ali Ipek alisisitiza dhamira ya Uturuki kuimarisha biashara, uwekezaji na ushirikiano wa kiuchumi hasa katika miundombinu, kilimo, nishati na teknolojia.

IPEK alisema JTC itakuwa jukwaa la kuondoa vikwazo, kurahisisha michakato na kukuza biashara na uwekezaji baina ya Tanzania na Uturuki.

“Kamati ya Pamoja ya Biashara itakuwa jukwaa lenye nguvu la kuondoa vikwazo, kukuza uwekezaji, na kufungua fursa mpya kwa mataifa yote mawili,” alisema.

Habari Zifananazo

4 Comments

  1. I started using this remote work platform about a month ago, and honestly, I was surprised how simple it is. I’m now making 1170+ per week — just from my phone. No special skills, no interviews. If you’re looking for something real and flexible, I’ve shared all the info on my site.

    HERE☛ rb.gy/uvl61

    1. I’m making $23000 to $29000 a month working part time. I kept hearing other people tell me how much money they ws can make online so I decided to look into it. Well, it was all true and has totally changed my life. First month i received $24758 just working on the laptop for 3 hours per day.
      This is what I do…………www.get.money63.com

  2. I started using this remote work platform about a month ago, and honestly, I was surprised how simple it is. I’m now making 1170+ per week — just from my phone. No special skills, no interviews. If you’re looking for something real and flexible, I’ve shared all the info on my site.

    HERE☛>>>>>>> rb.gy/uvl61

  3. I’m making $23000 to $29000 a month working part time. I kept hearing other people tell me how much money they ws can make online so I decided to look into it. Well, it was all true and has totally changed my life. First month i received $24758 just working on the laptop for 3 hours per day.
    This is what I do…………www.get.money63.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button