Tanzania ya Samia na Tuzo za Ubora wa Utalii Duniani

“HATUWEZI kuzungumzia mafanikio ya sekta ya utalii pasipo kutambua jitihada za makusudi zilizofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan alipoamua kutoka ofi sini na kwenda kutengeneza fi lamu za kimkakati za ‘Tanzania: The Royal Tour’ na ‘Amazing Tanzania’.

Kutokana na jitihada zilizofanyika, watalii wa ndani na nje wameendelea kuiamini na kuichagua Tanzania kama nchi salama kutembelea ili kujionea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo. Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Ashatu Kijaji anasema hayo akiwa katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi alipoambatana watalii wa ndani 100 kutembelea hifadhi, kuaga mwaka 2025 na kukaribisha mwaka 2026.

Anasema sekta ya utalii ni moja ya sekta za kimkakati na kimageuzi, kutokana na kuwa na mchango mkubwa unaoonekana na unaopimika katika uchumi wa taifa. Kwa mujibu wa Dk Kijaji, filamu hizo zimeiweka Tanzania katika ramani ya dunia na jitihada za Rais Samia zimechangia ongezeko la watalii wa kimataifa kwa asilimia 132.1 kutoka watalii 922,692 mwaka 2021 hadi 2,141,895 mwaka 2024.

Anasema watalii wa ndani wameongezeka kutoka 788,933 mwaka 2021 hadi 3,218,352 mwaka 2024 na kufanya watalii waliotembelea vivutio mbalimbali nchini kufikia milioni 5.3, sawa na asilimia 116.02 katika kipindi hicho. Dk Kijaji anasema ongezeko hilo linaendana na ongezeko la mapato yatokanayo na shughuli za utalii kutoka Dola za Marekani bilioni 1.3 mwaka 2021 hadi Dola za Marekani bilioni 3.9 mwaka 2024.

Kwa mujibu wa waziri huyo, mafanikio hayo yanaifanya Tanzania kushika nafasi ya tisa duniani na ya tatu barani Afrika kwa ongezeko la mapato ya utalii baada ya janga la Covid –19 na kwamba, mafanikio ya serikali kupitia wizara hiyo ni mikakati ya kuendeleza uhifadhi na utalii nchini. Kwa takwimu za Januari hadi Novemba 2025, anasema idadi ya watalii imeongezeka kwa asilimia 9.02 hadi kufikia 2,097,823 ikilinganishwa na watalii 1,924,240 mwaka 2024.

Takwimu za sasa zinaonesha kuwa, sekta ya utalii inachangia takribani asilimia 25 ya mauzo ya nje ya nchi na takribani asilimia 17.2 ya Pato la Taifa. Dk Kijaji anasema wizara imeibua mazao mapya ya utalii ya kimkakati ambayo ni Utalii wa Mikutano na Matukio (MICE) na utalii wa fukwe na bahari, historia na urithi, michezo, utamaduni pamoja na ikolojia ili kuchechemua utalii zaidi nchini.

Anasema sekta hiyo inachangia zaidi ya ajira milioni 1.5 za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja, huku ikigusa Inaendelea Uk. 10wananchi wa kawaida wakiwemo waongoza watalii, wakulima, wafugaji, wasanii, mama lishe, madereva na wawekezaji wakubwa.

“Ni muhimu tukumbuke jambo moja la msingi kuwa, utalii hauwezi kustawi bila amani, usalama na utawala bora, misingi ambayo Tanzania imeendelea kuilinda kwa nguvu zote,” anasema Dk Kijaji. Fauka ya hayo, anasema sekta ya utalii inaendelea kuimarika kwa kasi kutokana na jitihada za serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi katika kuimarisha utangazaji wa kimkakati, kuboresha miundombinu ya barabara, viwanja vya ndege, reli, bandari na kuboresha mazingira ya uwekezaji.

Anasema ili kuimarisha ushindani wa Tanzania kwenye soko la utalii kimataifa, wasimamizi wote wa vituo vya utalii nchini pamoja na wakuu wa taasisi zilizo chini ya wizara hiyo wanapaswa kuhakikisha wanakuja na mazao mapya ya utalii yenye ubunifu.

Ubunifu huo ni tofauti na uliozoeleka na uwe unaoongeza muda wa mtalii kukaa nchini, kuongeza matumizi ya mtalii na kuvutia masoko mapya ya ndani na nje ya nchi. “Ni wajibu kwa wasimamizi wa hifadhi kuona yale mazao ya utalii ambayo yamekuwepo kwa muda mrefu yafanyiwe maboresho ya kimkakati ili yawe na mvuto mpya zaidi,” anasema Dk Kijaji.

Mikakati ya kuvifanya vivutio hivyo kujulikana na kufikika ni pamoja na kujenga miundombinu mipya na kuboresha iliyopo ili Tanzania iendelee kuwa kivutio cha kipekee, shindani na chenye ubunifu endelevu katika soko la utalii duniani. “Nihamasishe na kutoa wito kwa Watanzania wote kutenga muda na kuja kutembelea vivutio vyetu, pia taasisi zetu zinazohusika na masuala ya utalii zije na progamu maalumu zitakazowezesha Watanzania wa makundi mbalimbali kutembelea vivutio hivi,” anasema.

Anawahimiza wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya nchini kushiriki kikamilifu kuhamasisha utalii wa ndani katika maeneo yao, kama ishara ya kumuunga mkono mhifadhi na mwongoza watalii namba moja nchini, Rais Samia.

Kwa mujibu wa Dk Kijaji, hatua hiyo itawezesha kufikia lengo la watalii milioni nane ifikapo mwaka 2030, kama ilivyoelekezwa katika Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2025. Dk Kijaji anamshukuru Rais Samia kwa utayari na ujasiri wake wa kunyanyua sekta ya maliasili na utalii, jambo lililowezesha Tanzania kupata tuzo tano kubwa zinazohusiana na masuala ya utalii duniani kwa mwaka 2025.

Anazitaja tuzo hizo kuwa ni; ‘Kituo Bora Duniani kwa Utalii wa Safari (World’s Leading Safari Destination – Tanzania) na ‘Serengeti ni Hifadhi Bora Duniani’ (World Leading National Park – Serengeti National Park). Tuzo nyingine ni ‘Tanzania ni Kituo Bora cha Utalii Afrika (Africa’s Leading Destination – Tanzania), ‘Ngorongoro ni Kivutio Bora cha Utalii Afrika (Best Tourist Atraction Ngorongoro) na ‘Zanzibar ni Kituo Bora cha Mikutano ya Mashirika na Mapumziko’ (African’s Best Cooperate Retreat Destination – Zanzibar).

Aidha, Dk Kijaji anasema katika Mwaka wa Fedha 2024/2025, serikali imewekeza zaidi ya Sh bilioni 284 kuimarisha miundombinu katika maeneo mbalimbali ya hifadhi. Anaitaja miundombinu hiyo kuwa ni pamoja na viwanja vya ndege, malazi kwa watalii na watumishi, kuboresha malango ya kuingilia wageni na vituo vya kutolea taarifa za watalii katika hifadhi za taifa Ruaha, Mikumi, Nyerere na Udzungwa.

Hivyo, anasema kutokana na jitihada hizo kubwa, Tanzania imeteuliwa kuwa mwenyeji wa tukio la utoaji tuzo za kimataifa kwa ngazi ya dunia zinazoitwa World Travel Awards (WTA) zinazotegemea kufanyika mwishoni mwa mwaka 2026. SOMA: Royal Tour inavyoakisi utalii wa Tanzania kimataifa

Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, Augustine Massesa anasema kujengwa miundombinu ya Reli ya Kisasa (SGR) kumewezesha hifadhi hiyo kuwa wanufaika wakubwa kwa kupata watalii wa ndani na nje. Kwa mujibu wa Massesa, uwepo uwanja wa ndege ndani ya hifadhi hiyo umeongeza idadi ya watalii sambamba na kuwepo malazi kunakomwezesha mtalii kupata mazingira mazuri ya kufanya utalii ndani ya hifadhi, na wengine kulala kwa sababu miundombinu ni rafiki.

Diwani wa Viti Maalumu, Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, Madina Fentu ni miongini mwa watalii 100 wa ndani waliotembelea hifadhi hiyo siku ya kuaga mwaka 2025 na kukaribisha mwaka 2026. Madina anasema kwa kutembelea hifadhi hiyo, amepata elimu kubwa zaidi ya matarajio yake. “Nilitarajia kuburudika zaidi na si kupatiwa elimu ya kujua utofauti wa tabia za wanyama, mimea na maisha yao kwa ujumla.

Nimepata elimu ya historia zao kutoka kwa wwalivyomwona simba na wanyama wengine katika uhalisia wao…” anasema Madina. Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima anasema mkoa huo umekuwa kituo kikuu cha utalii wa ndani unaochangiwa na miundombinu ya kisasa, hasa ya barabara na SGR. Malima anasema miundombinu hiyo rafiki na mingine ikiwamo ya ndani, imewarahisishia watalii wa ndani na nje ufikiaji wa vivutio vya utalii vilivyopo mkoani kwa wakati na kwa urahisi.

Kwa mujibu wa Malima, Mkoa wa Morogoro una vivutio vingi vya utalii vinavyopatikana katika hifadhi za taifa za Mikumi, Udzungwa na Nyerere pamoja na Pori la Akiba la Wami Mbiki linalosimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) pamoja na vivutio vingine vingi vikiwamo vya malikale. “Kwa sasa, mkoa umetangaza nafasi ya uwekezaji katika maeneo ya Doma katika wilaya za Mvomero na Kilosa, hivyo tunaiomba Wizara ya Maliasili na Utalii iyabebe malengo haya na kuyatangaza,” anasema.aongoza watalii; namna wanavyoishi mfano walivyomwona simba na wanyama”.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ https://Www.Jobathome1.Com

  2. l Get paid over $110 per hour working from home. l never thought I’d be able to do it but my buddy makes over $21269 a month doing this and she convinced me to try. The possibility with this is endless….

    This is what I do………………………………….. https://Www.Cash54.Com

  3. I am making a real GOOD MONEY (300$ to 400$ / hr )online from my laptop. Last month I GOT check of nearly 18,000$, this online work is simple and straightforward, don’t have to go OFFICE, Its home online job. At that point this work opportunity is for you.if you interested.simply give it a shot on the accompanying site….Simply go to the BELOW SITE and start your work…

    This is what I do………………………………….. ­­­ https://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button