Tanzania yahudumia zaidi ya 900 moyo, mifupa Zambia

WANANCHI zaidi ya 911  wamepata huduma za afya za kibingwa na bobezi kutoka Tanzania katika Maonesho ya Kilimo yaliyofanyika kuanzia Julai 29 hadi Agosti 4, 2025 mjini Lusaka nchini Zambia.

Katika maonesho hayo ya kilimo Tanzania iliibuka mshindi wa pili kati ya nchi 25 zilizoshiriki, ambapo Zimbabwe ilishika nafasi ya kwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati akitoa tathmini ya maonesho hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo (MOI) Dk Mpoki Ulisubisya amesema lengo kuu ni kubadilishana uzoefu katika utoaji wa huduma za matibabu na Bingwa.

Amesema ubalozi wa Tanzania nchini Zambia uliandaliwa na Maonesho ya Mabingwa na Usafirishaji yanayopatikana hapa nchini.

“Watu walitembelea maonyesho hayo. Balozi anafanya kazi ya kuzungumza na Wizara ya Afya ya Zambia ili madaktari waweze kuona watu na wale wanaohitaji kuja hapa,” amesema.

Amesema katika maonesho hayo Rais wa Zambia Hakainde Hichelema alitembelea mabanda ya Tanzania Agosti 2 na kupewa maelezo ya kina kuhusu huduma zinazotolewa.

“Taasisi ya Moyo (JKCI) ambayo imekuwa ikifanya kazi nchini Zambia tayari imefahamika kwa michango inayoshirikiana na Hospitali ya Moyo ya Zambia kusaidia watoto, lakini sasa wameonesha hata wazee wanaojali huduma hiyo,” amesema.

Amesema wagonjwa wengi walikuwa na matatizo ya moyo na kufuatiwa na matatizo ya mifupa katika sehemu mbalimbali za mwili.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na Mwenyekiti wa Utalii wa matibabu, Dk Peter Kisenge amesema sababu kubwa ya kushiriki ni kutoa tiba ya utalii ambapo Rais Samia Suluhu Hassan amewekeza zaidi na amewekeza kwenye sekta ya afya ili wananchi wa nje wapate matibabu.

“Tulipata zaidi ya watu 900 waliotembelea mabanda hayo na waliona kazi iliyofanywa na serikali zetu walihisi huduma zinazotolewa India ziko Tanzania na waliona gharama ya Tanzania ni nafuu kuliko kwenda India,” amesema.

Dk Kisenge amesema wananchi wanajiandaa na matibabu ya utalii yanaongezeka kwa hoteli, wafanyabiashara na wengine watakaokwenda kwenye mbuga za wanyama hivyo wanataka Tanzania iwe Afrika India.

 

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button