Tanzania yavutia wadau maonyesho Qatar 2025

QATAR: TANZANIA imevutia wadau wengi wa biashara katika maonyesho ya Project Qatar 2025, yaliyoanza Mei 26 yanayotarajiwa kumalizika Mei 29, 2025 kwenye ukumbi wa maonyesho na mikutano wa Doha (DECC) Doha, nchini Qatar.

Tanzania imeshiriki maonyesho hayo kwa kushirikiana na ujumbe unaowakilisha wadau wa sekta ya umma na binafsi kutoka sekta ya ujenzi na viwanda ikiwemo Wizara ya Ujenzi, Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Wakala wa Majengo (TBA).

Wengine ni wawakilishi kutoka Bodi ya Usajili ya Wabunifu na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) na Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB wakandarasi binafsi na kampuni ya ushauri wa kihandisi.

SOMA ZAIDI: Wadau 800 nchi 40 duniani kushiriki maonyesho KKF

Aidha, katika maonyesho hayo yaliangazia shughuli za maendeleo ya kikanda katika ujenzi, pia ubunifu wa kiteknolojia na mifumo mahiri inayobadilisha tasnia ya utengenezaji bidhaa ulimwenguni.

Hafla hiyo ilizinduliwa rasmi Mei 26 2025, na Naibu Katibu Msaidizi wa Maendeleo ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Biashara na Viwanda, Saleh bin Majid Al-Khulaifi.

Aidha, maonyesho hayo yalivutia washiriki kutoka sehemu mbalimbali duniani, wakiwakilisha sekta mbalimbali zikiwemo ujenzi, viwanda, uhandisi, ushauri, upimaji wingi, usanifu na maendeleo ya biashara.

Ushiriki huo unaashiria hatua kubwa katika kuimarisha uwepo wa Tanzania katika masoko ya kikanda na kimataifa ya ujenzi na viwanda, na hivyo kuimarisha dhamira ya nchi katika uvumbuzi na maendeleo endelevu.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button