TAP TAP UTOBOE: Kuwajaza wateja fedha, bajaji na gari

Dar es Salaam: BENKI ya Exim Tanzania imezindua kampeni maalum inayolenga kuwashawishi wateja wake wanaomiliki simu za mkononi kufanya miamala zaidi kwa kutumia simu zao pamoja na kutumia mtandao badala ya malipo ya fedha taslimu pindi wanapohitaji kutumia huduma mbalimbali za kibenki.

Kampeni hii ya miezi mitatu itaambatana na zawadi mbalimbali ambazo zitatolewa kila wiki na mwezi kwa washindi.

Kampeni hiyo iliyopewa jina la ‘Tap Tap Utoboe’ inatoa fursa kwa zaidi ya washindi 200 miongoni mwa wateja wa benki hiyo wanaotumia simu zao au mtandao kufanya miamala, kuwa kwenye nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslimu, pikipiki, bajaji pamoja na zawadi kubwa ya gari mpya aina ya Mazda CX-5.

Tap Tap Utoboe inalenga wateja wa sasa na wateja wapya ambapo kwa mteja ambaye hajawahi kutumia huduma za kibenki za simu za mkononi na mtandaoni, hii ni fursa yake kujiunga.

Kwa wateja wapya, wanaalikwa kujiunga na familia ya Exim Bank ili kufurahia huduma bora za kibenki za kidigitali. Ili kushiriki, mteja anatakiwa kufanya miamala yake yote ya kibenki kupitia simu yake au mtandao, ikiwamo kulipia ankara za maji, umeme au visimbusi vya television, malipo ya manunuzi, kutuma pesa, kulipia kodi, kutoa fedha kwa Exim Wakala, kulipia bima ya vyombo vya moto na huduma nyenginezo.

Stanley Kafu, Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim (kulia), mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Lucy Obadia Katamba (katikati), Andrew Lyimo, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo na wa Kati, na Silas Matoi, Mkuu wa Njia Mbadala na Mabadiliko ya Kidijitali (kushoto), wakiwa katika uzinduzi wa kampeni ya ‘Tap Tap Utoboe’. Kampeni hii inahimiza wateja kufanya miamala zaidi kwa kutumia simu za mkononi na majukwaa ya mtandaoni badala ya malipo ya pesa taslimu. Tukio hilo lilifanyika katika makao makuu ya benki hiyo tarehe 10 Juni, 2024. Wateja watapata nafasi ya kushindia fedha taslimu kila wiki na mwezi, pikipiki, bajaj, na mshindi wa kwanza atashindia gari mpya aina ya Mazda CX 5.

Ili kushinda zawadi, mteja anahimizwa kufanya miamala ya mara kwa mara kupitia huduma za kibenki za simu za mkononi na mtandaoni. Washindi kumi wa kila wiki watapata 50,000/- kila mmoja, na washindi kumi wa kila mwezi watapata TZS 100,000 kila mmoja.

Mshindi wa tatu atapata pikipiki, mshindi wa pili atapata bajaji, na mshindi wa kwanza na jumla ataondoka na gari mpya kabisa aina ya Mazda CX-5.

Kwa mujibu wa Exim Bank wakati wa kampeni hiyo kila muamala wenye thamani ya Tsh 50,000/= na zaidi ukiwa umefanyika kwa zaidi ya mara moja kupitia simu ya mkononi au mtandao, muhusika atastahili kushiriki bahati nasibu ya kumpatia mshindi.

Silas Matoi, Mkuu wa Njia Mbadala na Mabadiliko ya Kidijitali, alisema, “Ubunifu wa kidijitali ni msingi wa mkakati wetu. Kampeni ya Tap Tap Utoboe imeundwa kuhusisha watumiaji wa teknolojia na wale wasioijua sana, kuhakikisha kila mmoja anafaidika na huduma zetu.”

“Kila wiki, kutakuwa na droo na wateja 10 watakaobahatika watapata nafasi ya kujishindia zawadi ya fedha taslimu 50,000/-.’’ Alitaja, huku akiongeza: “Aidha, kila mwezi kutakuwa na droo ambapo wateja 10 watapata nafasi ya kujishindia fedha taslimu 100,000/- huku sifa ya chini katika droo hii ya mwezi ikiwa ni mhusika kufanya miamala yenye thamani ya 200,000/- na zaidi katika huduma moja au zaidi.” anaongezea Silas.

Akizungumzia zawadi kuu kwa washindi wa kampeni hiyo, Silas alisema “Hivyo basi mshindi wa kwanza atajishindia zawadi ya gari mpya kabisa aina ya Mazda CX-5 ambayo iko tayari kuingia barabarani ikiwa na bima kubwa. Mshindi wa pili ataondoka na Bajaj na mshindi wa tatu atajipatia pikipiki ambavyo pia vina bima kubwa.

Kupitia kampeni hii ya ‘Tap Tap Utoboe’, Exim Bank inalenga kukuza uchumi jumuishi kwa kuwapa wateja fursa sawa za kupata huduma za kifedha. Huduma za kibenki za simu na mtandaoni za Exim Bank zinatoa fursa kwa watu wote, wakiwemo wale wa vijijini, kupata huduma za kibenki kwa urahisi zaidi. Hii inasaidia kuongeza ushirikishwaji wa kifedha na kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika jamii.

Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki hiyo Bw Stanley Kafu alisema dhamira ya msingi ya benki hiyo ni kuandaa jamii yenye utamaduni wa kutotembea na pesa taslimu na badala yake wafanye miamala kwa njia za kielectroniki hatua ambayo pia imekuwa ikipigiwa chapuo na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya kidunia katika kufanya miamala ya kifedha.

“Tunajivunia ushirikiano wetu na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania katika kampeni hii. Ushirikiano huu ni endelevu na unalenga kuhakikisha kampeni hii inafanyika kwa ubora na ufanisi mkubwa” aliongeza.

“Benki yetu kihistoria imekuwa mstari wa mbele kuleta mageuzi ya kihuduma hapa nchini. Katika kufanikisha mageuzi hayo tumekuwa tukitumia namna mbambali ikiwemo kutoa zawadi kwa wateja wetu ili tu tuweze kwenda nao sambamba katika mageuzi haya.

“Tunaamini kupitia kampeni hii tunakwenda kuleta mabadiliko yenye tija na faida kubwa kwenye mfumo mzima wa sekta ya fedha hapa nchini na iatawapa wateja wetu fursa ya kufurahia huduma za kibenki zenye urahisi wa matumizi, upatikanaji wa haraka, na uaminifu. Hii ni sehemu ya kujitolea kwetu katika kuboresha huduma kwa wateja wetu na kuwahamasisha kutumia huduma zetu za kidijitali,’’ alisema.

Habari Zifananazo

Back to top button