TCB yaondoa hofu upatikanaji mbegu bora za pamba

BODI ya Pamba Tanzania (TCB) imewatoa hofu wakulima wa zao hilo juu ya upatikanaji wa mbegu bora za kisasa za pamba katika msimu mpya wa kilimo 2025/2026.

Wakulima wametakiwa kutokuwa na hofu yoyote, kwani bodi hiyo imejipanga vya kutosha na kubainisha kuwa asilimia zaidi ya 80 ya mbegu zote zinazohitajika katika msimu wa mwaka huu tayari zimezalishwa.

Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea Kiwanda kinachozalisha mbegu hizo mkoani Shinyanga cha Jeylong, Mkaguzi wa Pamba kutoka bodi hiyo, Thadeo Mihayo alisema hakuna mkulima atakayekosa mbegu.

Thadeo alisema katika kiwanda hicho zaidi ya asilimia 90 ya mbegu zimezalishwa na kuanza kupelekwa kwa wakulima, ambapo alitaka kampuni za ununuzi wa zao hilo ambazo zimepewa kazi ya kusambaza mbegu kuhakikisha wanatekeleza wajibu huo.

SOMA: Wakulima wa pamba ‘wanavyolia’ bei kupata tija

“Niwatoe hofu wakulima wa pamba, Bodi ya Pamba imejipanga vya kutosha kuhakikisha kila mkulima anapata mbegu kulingana na mahitaji yake. Wakulima watapata mbegu hizi ndani ya muda mwafaka, hazitachelewa,” amesema.

Amesema bodi imepeleka kiwandani hapo mbegu za pamba zenye manyonya ili kuchakatwa Kilogramu milioni 12, huku lengo likiwa ni Kilogramu milioni 13 ambapo mbegu Kilogramu milioni 5.8 tayari zimechakatwa.

Aidha, Thadeo amesema kuwa mbali na mbegu nyingi kuzalishwa lakini pia wakulima watapata mbegu hizo kwa wakati na muda mwafaka kwenye maeneo yao kabla ya msimu wa kupanda haujafika.

Ameongeza kuwa, mbegu zinazotoka Kiwanda cha Jeylong zinahudumia wakulima wa mikoa ya Shinyanga,
Katavi, Kigoma, Tabora, Singida, Dodoma na Ukanda wa Mashariki pamoja na Mkoa wa Simiyu Wilaya ya Meatu.

Ameongeza: “Tunataka zile kampuni ambazo tumezipa kazi ya kusambaza mbegu kuhakikisha wanatekeleza wajibu huo. Baadhi ya mbegu tayari zimepelekwa kwa wakulima na nyingine zinaendelea kupelekwa, hivyo wakulima wasiwe na wasiwasi.”

Mkulima Masaka Seni amesema, “Msimu wa mwaka huu, wakulima wengi tumejipanga kuzalisha kwa tija na kulima kitaalamu. Tunachokiomba kwa serikali ni kutuwahishia mbegu za pembejeo nyingine kama dawa za wadudu”

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button