TCRA yatahadharisha uchochezi habari za uchaguzi

DAR-ES-SALAAM : MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewataka waandishi wa habari waepuke kuripoti taarifa za uchochezi zinazoweza kuchochea migogoro na vuruga amani wakati wa Uchaguzi Mkuu.
Meneja wa Huduma za Habari za Utangazaji TCRA, Andrew Kisaka amesema hayo jijini Dar es Salaam katika mkutano wa wadau wa sekta ya habari na utangazaji Kanda ya Mashariki kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025.
Kisaka alisema vyombo vya habari vinapaswa kufahamu na kuzingatia wajibu wao wakati wa uchaguzi ambao ni kutopendelea wakati kutoa taarifa, kuhakikisha uwazi kwenye mchakato wa kisiasa, kutoa jukwaa kwa wagombea na wapigakura kujadili mada muhimu.
Alisema ili kuepuka kufanya uchochezi waandishi wa habari wanapaswa kuzingatia na kujua viashiria vya migogoro vikiwemo vitisho, manyanyaso na vurugu dhidi ya baadhi ya makundi, maneno ya chuki kuwalenga wagombea, wapigakura au vyama vya siasa kwa vitisho na hofu na kushambulia mchakato wa upigaji kura katika vituo vya kupigia kura, viongozi wa maamuzi.
Kwa upande wake, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM), Dk Egbert Mkoko amesema ni muhimu kwa waandishi wa habari kuzingatia mwongozo wa habari katika kuripoti Uchaguzi na kukabidhi nyaraka ajaze kwa mujibu wa sheria, kanuni na utaratibu.
Mgombea mwingine aliyekabidhiwa fomu za uteuzi kugombea ubunge Jimbo la Mvomero ni wa Chama cha Democratic Party (DP), Fatuma Mohamed. Pia, msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo jana alikabidhi fomu ya uteuzi kwa mgombea wa ubunge ku- pitia Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT Wazalendo), Kashikashi Ligowoka.
Kayowa aliwahakikishia wagombea hao kuwa INEC ni chombo huru kilichojipanga kuzingatia katiba, sheria na kanuni wakati wote wa mchakato wa Uchaguzi Mkuu. SOMA : Dhamana ya vyombo vya habari wakati wa uchaguzi



