Teknolojia mifumo ya benki yaendelea kuinua uchumi

UWEPO wa matumizi ya teknolojia kupitia mifumo ya benki umepelekea wananchi kufanya miamala kupitia simu zao maeneo ya mijini na vijijini ikiwemo kuinua uchumi kupitia sekta za fedha.

Hayo yamesemwa na Ofisa Mkuu wa Biashara kutoka Benki ya CRDB, Boma Rabala wakati akielezea umuhimu wa matumizi ya telnolojia katika udhibiti mianya ya wizi wa mitandao katika mkutano wa pili wa mwaka wa Jumuiya ya Wahasibu Wakuu wa Nchi za Afrika (AAAG) unaofanyika jijini Arusha.

Amesema banki hiyo imedhamini mkutano huo kutokana na umuhimu wake ili waweze kuwa karibu na wahasibu hao ambao ni wataalam wa fedha ili kujifunza masuala mbalimbali yakiwemo udhibiti wa matumizi yasiyo sahihi ya telnolojia yanayoleta athari katika miamala ya utoaji wa fedha kwa wateja na matumizi sahihi ya mitandao.

Amesema kutokana na ukuaji wa telnolojia wananchi wengi wamejiunga na huduma za simu ikiwemo kuhamisha miamala ya simu kutoka benki  kwenda kwenye simu za kiganjani hiking benki hiyo ikiongoza kutoa huduma mbalimbali kwa wateja.

Naye Waziri wa Fedha akishiriki mkutano huo, Mwigulu Nchemba amesisitiza umuhimu wa teknolojia na ubunifu katika kuboresha mifumo ya kifedha barani Afrika ili kukabiliana na changamoto mpya zinazojitokeza kutokana na maendeleo ya Tehama duniani.

Mkutano huo wa AAAG unatarajiwa kutoa mapendekezo muhimu yatakayosaidia kuboresha usimamizi wa fedha za umma katika nchi za Afrika kwa ustawi wa kiuchumi wa bara zima umewaleta  pamoja wataalam wa usimamizi wa fedha kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika kwa lengo la kubadilishana mawazo na kuboresha mifumo ya kifedha.

Habari Zifananazo

Back to top button