TET watoa mafunzo mtaala ulioboreshwa
DAR ES SALAAM: Katika kuelekea siku ya Wanawake Duniani Wakuza Mitaala wanawake kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) wametoa mafunzo ya mtaala ulioboreshwa kwa walimu wa baadhi ya shule za Jiji la Dar es Salaam.
Mafunzo hayo yametolewa leo Machi 6, 2024 kama sehemu ya kuadhimisha siku hiyo itayofanyika kesho Machi 8, 2924.
Mafunzo hayo yamefanyika katika shule za msingi za Oysterbay, Olimpio, Buguruni, Kunduchi, Mivumoni, Kimwani, Chamazi, Majimatitu, Mikwambe, Kigogo, Raha Leo, Kimbiji, King’azi, Tegeta na Anazaki.
Lengo ni kujadiliana mbinu mbalimbali za kufundishia wanafunzi kuhusu Mtaala ulioboreshwa.
Katika majadiliano hayo, walimu kutoka shule hizo walipata nafasi ya kuujua Mtaala ulioboreshwa kwa undani na kutoa mawazo mbalimbali ya namna bora ya kuboresha mbinu za ufundishaji ili Mtaala huo ulete tija kwa mwanafunzi.