Tetesi za usajili Ulaya

Soccer Football - LaLiga - Real Madrid v FC Barcelona - Santiago Bernabeu, Madrid, Spain - October 16, 2022 FC Barcelona's Sergio Busquets shakes hands with coach Xavi as he is substituted REUTERS/Juan Medina

KIUNGO wa Ujerumani, Jamal Musiala amekataa kandarasi mpya katika klabu ya Bayern Munich huku akilenga kuhamia Ligi Kuu England msimu wa joto, huku Manchester City na Liverpool wakiongoza katika kinyang’anyiro cha kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21, mtandao wa Star unaripoti.

Meneja Thomas Tuchel huenda akafutwa kazi ikiwa Bayern Munich itapoteza mchezo wao wa mkondo wa 16 bora wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Lazio Jumanne.

(Sky Sports Ujerumani)

Advertisement

Meneja wa Manchester United Erik ten Hag anamfuatilia beki wa Girona Mhispania Miguel Gutierrez, 22 kabla ya dirisha la usajili la kiangazi. (Sun)

Liverpool wamezidisha nia yao ya kutaka kumnunua kocha mkuu wa Sporting Lisbon Ruben Amorim, lakini kocha wa Bayer Leverkusen Xabi Alonso anasalia kuwa mstari wa mbele kuchukua nafasi ya Jurgen Klopp. (Mirror)

Matumaini ya Barcelona kumteua mkufunzi wa Brighton Roberto de Zerbi msimu wa joto yametatizwa na kukataa kwa ‘Seagulls’ kufanya mazungumzo juu ya kipengele cha kutolewa cha Euro 15m. (Sport)

Klabu ya Barcelona imefanya mazungumzo na kocha wa zamani wa Ujerumani Hansi Flick kuhusu kurithi mikoba ya Xavi. (Florian Plettenberg)

Mshambuliaji wa Paris St-Germain na Ufaransa Kylian Mbappe amekutana na Luis Enrique ili kutatua mvutano unaotokana na kocha mkuu wa Uhispania kumbadilisha mchezaji huyo wa miaka 25 katika michezo wa juzi. (ESPN)

Fulham, Everton, West Ham na Wolves wanamfuatilia winga wa Galatasaray mwenye umri wa miaka 31 wa Ivory Coast Wilfried Zaha. (Ekrem Konur)

Barcelona itaweka kipaumbele katika kuwauza winga wa Brazil Raphinha, 27, na mlinzi wa Ufaransa Jules Kounde, 25, msimu wa joto. (Sport)