THRDC yapinga kukamatwa Wakili Mahinyila

DAR ES SALAAM – Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umelaani kukamatwa kwa Wakili Deogratius Mahinyila ndani ya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam, ukisema kitendo hicho kinadhoofisha heshima na hadhi ya mawakili nchini.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Septemba 24, jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Mtandao huo Kitaifa, Wakili Onesmo Olengurumwa amesema “kitendo hicho hakikuwa sahihi” akifafanua kuwa Mahanyila alikuwa akitekeleza majukumu yake.

Tamko la THRDC linakuja siku chache baada ya Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) kutoa msimamo tata wa mawakili kuungana na kulaani kukamatwa kwa Wakili Mahinyila. Msimamo huo ulipingwa na Chama cha Mawakili wa Serikali (PBA).

“Uamuzi huo pia ulikuwa ni sehemu ya kulinda heshima ya taaluma ya sheria na kuonesha mshikamano wa kitaaluma pale ambapo mwanachama mmoja anakumbwa na changamoto zinazoweza kudhoofisha uwezo wake wa kutekeleza wajibu wake kisheria,” amesema Wakili Olengurumwa.

Akisisitiza kuwa ni wajibu wa vyama vya wanasheria na taasisi za haki za binadamu kuhakikisha mazingira ya mawakili kufanya kazi zao bila hofu, kwani mazingira hayo ndiyo msingi wa haki na usawa mbele ya sheria.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button