Timu ya MSLAC yamsadia mtoto Loveness kuanza shule

TIMU ya Uratibu wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia imetatua changamoto ya mtoto Lovenes ,13, anayeishi kijiji cha Bubale kilichopo wilayani Missenyi mkoani Kagera ambaye hajawahi kwenda shule kutokana na wazazi wake kuhamahama makazi kufuata ajira ndani na nje ya nchi.
Aidha kwa sasa timu hiyo imetimiza hitaji lake la kujiunga na elimu ya watu wazima katika Shule ya Msingi ya Bubale wilayani Missenyi.
Mtoto Lovenes aliwafuata waratibu wa kampeini ya msaada wa kisheria na kuwapigia magoti kwa kusema kuwa kama atafanikiwa kuanza shule na kupata elimu ya watu wazima akajua kusoma na Kuandika atasimulia maisha yake yote kuwa kampeini hiyo iliwai kumuletea mafanikio makubwa maishani mwake.
“Simujui baba yangu na mama yangu yuko nchini Uganda, nimeishi maisha ya kuhamahama na nimekuwa mtumwa wa kazi za ndani ,mjomba wangu ameniokoa kutoka kwenye utumwa wa kazi za ndani, matumaini yangu leo ni kuunganishwa na mwalimu ili niende shuleni, kama nitaanza shule nikajua kusoma na kuandika basi itakuwa simulizi maisha yangu yote,”amesema.
Loveness alionekana mtoto peke yake kati ya mamia waliokusanyika kupata huduma za msaada wa kisheria lakini amesema kama timu inaweza kununua vifaa vya shule na akajua kusoma na Kuandika pamoja na kuamka kwenda shuleni kama watoto wengine basi hataweza kusahau jina linaloitwa Mama Samia.

Lovenes alimwambia mratibu wa Kampeini ya Msaada wa Kisheria wilayani Missenyi kuwa hajawai kumujua baba yake isipokuwa mama yake ambaye anakimbia mara nyingi na kumuacha pamoja na mjomba wake ambaye sasa amemuondoa sehemu za mateso alikokuwa ameajiliwa na mtu maeneo ya Kagera Sukari.
“Sijui Kuandika jina langu wala la baba yangu, sijui chochote moyoni mwangu nilifikiria kwamba kama wageni wanaokuja wanasikiliza changamotoo za watu wenye matatizo basi na mimi kama mtoto nitajipeleka niwasilishe tatizo langu la kipekee ili iwe mara yangu ya kwanza kusaidiwa kutimiza ndoto yangu ya kusoma na naomba mnisaidie niende shuleni nikasome na mimi,”alisema
Mratibu wa kampeini ya msaada wa kisheria ya Mama Samia wilayani Missenyi Maximilian Fransis baada ya kupokea kilio icho aliwasiliana na mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Rubale ambapo amesema yupo tayari kumpokea na kumusajili shuleni kwa mfumo wa elimu ya watu wazima.
Mratibu huyo pia na wajumbe wa kamati wamehakikisha mtoto huyo anapata mahitaji yote ya shule ambapo amenunuliwa madafutari ,sare za shule, pesa ya viatu, na sweta ili kuanza safari yake ya kusoma.
Mjomba wa Mtoto huyo Enias amesema kuwa yeye anazaliwa na dada zake wawili dada yake mmoja amepotelea nchini Uganda na mwingine amefariki hivyo baada ya kupata taaarifa kuwa wanawatoto alianza kutafuta namna ya kuwa weka pamoja na kuwatoa kwenye mateso.
Alisema kuwa kampeini hiyo itafanya hata watoto waliokwama na waliositishwa masomo kurudi shuleni ili watimize ndoto zao huku akihaidi kuwalea watoto wa dada zake kama mzazi na kuwasahahulisha manyanyaso ambayo wamekuwa wakiyapitia huko nyuma.
Alitoa shukurani kwa serikali ya Mama Samia kwa kuibua changamoto na kuwafata wananchi katika vijiji vya pembezoni ,kwani wanachangamoto nyingi za kisheria na hawana gharama za kuwalipa mawakili ili kushinda kesi zao.



