TMDA yatahadharisha matumizi holela ya Dawa

DAR-ES-SALAAM : MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imetoa tahadhari kwa wananchi dhidi ya matumizi holela ya dawa bila ushauri wa wataalamu wa afya, hatua inayoweza kusababisha usugu wa vimelea na kuathiri ufanisi wa matibabu.
Akizungumza wakati wa Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara (Saba Saba), Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Adam Fimbo alisema mamlaka hiyo inaendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu matumizi sahihi ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi ili kulinda afya ya jamii.
“TMDA inatekeleza jukumu la kusajili dawa, vifaa tiba na vitendanishi vinavyozalishwa ndani na vinavyoingizwa kutoka nje ya nchi. Tunahakikisha bidhaa hizo ni salama, bora na zenye ufanisi kabla ya kuruhusiwa kutumika nchini,” alisema Fimbo.
Alieleza kuwa TMDA hufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika maduka ya dawa, masoko na maeneo ya mipakani ili kudhibiti uingizaji na usambazaji wa dawa zisizofaa. “Tunaendelea kutoa elimu kwa wananchi kupitia maonesho haya na majukwaa mengine ili kuhakikisha jamii inatambua madhara ya kutumia dawa bila ushauri wa wataalamu wa afya,” aliongeza.
Alisisitiza kuwa matumizi sahihi ya dawa ni msingi wa matibabu bora na kwamba kila Mtanzania anapaswa kuchukua tahadhari ili kujikinga na athari zinazoweza kusababishwa na matumizi mabaya ya dawa.SOMA: Mambo 12 ya TMDA miaka minne ya Samia
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily…. Www.JoinSalary.Com
I get paid over $130 1 to 3 hours working from home with 2 kids at home. I never thought I’d be able to do it but my best friend earns over $27k a month doing this and she convinced me to try. The potential with this is endless.
Heress———–> http://www.now.jobs67.com