TOSCI yahimiza usajili wa miche ya parachichi

DAR-ES-SALAAM : MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya kudhibiti ubora wa mbegu Tanzania (TOSCI) Nyasebwa Chimagu amesema wzalishaji na wauzaji wa miche ya parachichi  wanatakiwa kusajili mashamba ya miti mama ya parachichi kwaajili ya uzalishaji wa vikonyo ,kusajili vitalu vya uzalishaji wa miche bora ya kubebesha  na kusajili vitalu vya uzalishaji wa miche bora iliyobebeshwa.

Katika taarifa iliyotolewa leo na TOSCI kwa waandishi wa habari hadi sasa  mbegu za miche ya parachichi iliyosajiliwa ni aina tano ambazo ni HASS,PINKERTON,FUERTE,X-IKULU na BOOTH 7 ili kuwezesha wakulima kupata miche yenye  ubora iliyothibitishwa hivyo kuongeza tija na kipato.

“Serikali kupitia wizara ya kilimo imeendelea kulipa kipaumbele zao la parachichi  kutokana na mchango wake katika lishe ,ajira kwa vijana na wanawake ,biashara ya pamoja  na kuongeza mapato ya fedha za kigeni nchini. SOMA: Wakulima kunufaika ruzuku mbegu bora, pembejeo

Ameongeza “TOSCI inakumbusha wazalishaji na wauzaji wa miche ya parachichi kuwa kwa mujibu wa sheria ya mbegu sura ya 308 na kanuni na sheria za mbegu za mwaka 2007  mbegu zote zinazouzwa ni lazima ziwe zimethibitishwa ubora.

Aidha amesema  ili kuendana na malengo ya serikali ya kuwezesha wakulima kupata miche bora ya parachichi wazalishaji ,wauzaji na wauzaji wa miche ya parachichi wanatakiwa kutekeleza sheria. Ameeleza kuwa usajili huo unatapaswa kufanyika ndani ya siku 90 kuanzia Septemba 23,2025 na baada ya muda huo kupita TOSCI itawachulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika kukiuka utaratibu huo .

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button