TRA Kagera watoa elimu ya kodi kwa wafanyabiashara

KAGERA: VIONGOZI kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na maofisa wake mkoani Kagera wamefungua maadhimisho ya ‘Juma la Huduma Bora’ kwa wateja na kuwatembelea wafanyabiashara mkoani humo ili kutoa elimu ya kodi na kusikiliza changamoto za kikodi.
Naibu Kamishina wa Upelelezi wa Kodi, Hashimu Ngoda amewaongoza viongozi mbalimbali na maofisa waandamizi kwa kuwafikia wafanyabiashara mkoani Kagera na kutoa elimu huku wafanyabiashara hao wakiombwa kuongelea kero na kuwasilisha changamoto.
Kupitia ‘Juma la Huduma Bora’ kwa wateja viongozi wa TRA wameyafikia makundi ya wafanyabiasha mbalimbali na kusisitiza matumizi ya risiti za kielectroniki katika bidhaa wanazouza na huduma wanazotoa huku akisisitiza kuwa TRA imejipanga kushughulikia kero za wafanyabiashara.
“Tumetumia juma la huduma kwa mlipa kodi kusikiliza changamoto za wateja na kutoa elimu lakini pia kuwasihi wateja kuondoa woga tuko tayari kuwahudumia kwa kuwasikiliza kwa njia zote nzuri, kuna mabadiliko makubwa sana kwa TRA ukilinganisha na miaka iliyopita wafanyabiashara wasiogope kama wamekwama waje tuzingumze,” alisema Ngoda.
Pamoja na mambo mengine viongozi hao wamewasisitiza wafanyabiashara wa mkoa wa Kagera kutumia mipaka Halali ya kupitisha mizigo ya biashara ili kuepusha changamoto za kufirisiwa kwani wafanyabiashara wanaopitisha mizigo vichochoroni wakikamatwa mizigo yao yote inataifishwa.
“Tumeboresha sana mipaka yetu ,tumeajili maofisa wabobezi na wasikivu tumasikiliza wateja masaa yote ,tumeondoa changamoto zote hili kuepusha fikra za magendo hakuna haja ya kufanya magendo Tujikite katika Kufanya biashara halali na kujiepusha na kufanya biashara za Magendo,”alisema
Mmoja wa wafanyabiashara ambaye ametembelewa kisha Ilamulila ameipongeza TRA kwa kuendelea kuwasikiliza wafanyabiashara na kuwahudumia kwa wakati huku akiomba waendelee kutoa elimu bila kuchoka ili kila Mtanzania aweze kulipa kodi kwa hiari.
“Tunaipongeza serikali Kuna mabadiliko makubwa sana TRA wateja na TRA lengo letu ni moja Kupata Kodi na kuona miradi ikitekelezwa zamani wafanyabiashara walikuwa waoga hata kusogelea jengo lakini kwa sasa hakuna anayemuogopa mwenzake tumeelewana na tuko vizuri sana kinachotakiwa Kila mmoja aone umuhimu wa kulipa Kodi kwa hiari ili kufurahia matunda ya Kodi zetu”alisema Ilamulila
Juma la Huduma Bora kwa wateja litafikia tamani Oktoba 12 mwaka huu.