TRA wazindua mfumo wa tija ukusanyaji mapato

MAMLAKA ya Mapato Tanzania(TRA) imezindua Mfumo wa Usimamizi wa Maarifa unaoleta tija zaidi katika ukusanyaji mapato pamoja na rejea za kihistoria zinazosaidia watumishi kuusimamia vema ikiwemo kutoa makadirio ya kodi kwa wakati katika kuepuka mianya ya rushwa .
Akizindua mfumo huo jijini Arusha na Kamisha wa TRA, Yusuph Mwenda wakati wa uzinduzi wa mfumo huo ulioshirikisha mameneja wa TRA nchi nzima ambapo alisisitiza mfumo huo unaloteja tija na maarifa sahihi kwa kuweka utaratibu wa kuhifadhi taarifa katika sekta mbalimbali za uwekezaji, viwanda, biashara, wateja wa kila kada, utoaji wa mizigo inayoingia nchini na nk.
Amesema kazi ya TRA ni kukadiria, ukusanyaji wa mapato ya serikali huku akisisitiza katika kukadiria lazima kuwe na maarifa na taarifa za sheria za kodi, viwanda unavyoenda kukagua katika kuhakikisha uchumi unakua kwa ukusanyaji mapato na ukuaji wa uchumi kidigitali
Mamlaka hiyo imetii agizo la Rais Samia Hassan Suluhu aligiza TRA kutenda haki kwa walipakodi kwa kutowatolea makadirio makubwa wala madogo hivyo mfumo huu unajibu kwa vitendo utekelezaji wa agizo hilo kwa kuongeza maarifa kwa watumishi ikiwemo ulipaji kodi kwa walipakodi katika kuhakikisha kila mmoja anakadiriwa kodi na kulipa kwa wakati.
“Mfumo huu utatoa majibu ya kutopendelewa au kukadiriwa mapato kwa mlipa kodi lakini pia mfumo huo utaondoa mianya ya rushwa ikiwemo kutoa taarifa sanjari na kuona jinsi watumishi wanaojitolea kazini katika mchango endelevu wenye kuleta tija zaidi pamoja na kuongeza uwazi katika maamuzi ya kodi ikiwemo kuleta ushindani katika soko la Dunia”
Naye Naibu Kamisha Mkuu wa TRA, Mcha Hassan amesema mfumo huo ni miongoni mwa mfumo unaleta ufanisi katika kukuza teknolojia kupitia maarifa ili kujikita zaidi kiushindani.