TRA yaagizwa kukomesha matumizi mabaya ya misamaha ya kodi nchini

SERIKALI imeitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kukomesha matumizi mabaya ya misamaha ya kodi ili malengo ya serikali ya kuvutia wawekezaji zaidi yafi kiwe.

Waziri wa Fedha, Balozi Profesa Khamis Mussa Omar alitoa agizo hilo wakati akifungua Mkutano wa Tathmini ya Utendaji Kazi wa Nusu ya Mwaka wa Fedha 2025/2026 mkoani Arusha.

Profesa Omar aliitaka Wizara ya Fedha kushirikiana ipasavyo na TRA ili kufanikisha mapambano hayo dhidi ya matumizi mabaya ya misamaha ya kodi nchini.

Kadhalika, amefafanua kuwa misamaha ya kodi inalenga kukuza sekta ya uwekezaji ambayo inaongeza mapato ya nchi kupitia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

Alitoa ushauri kwa TRA kuendelea kuhimiza matumizi mazuri ya misamaha ya kodi kuendelea kuvutia uwekezaji mkubwa na kushajihisha ukuaji wa uchumi wa nchi.

Aidha, alitaka kauli na matamko yanayotolewa na viongozi wa TRA yalenge na kuzingatia majukumu ya TRA ya kukuza na kuvutia uwekezaji mkubwa ili kupata kodi kubwa.

“Kuna wakati katika kauli zetu tunatakiwa tuseme kuwa na sisi tuna jukumu la kuanzisha na kushajihisha uwekezaji mkubwa zaidi nchini ili kupanua ukusanyaji wetu wa kodi,” aliongeza Profesa Omar.

Aliitaka TRA kuimarisha zaidi Idara ya Utafiti ili ikae karibu na wadau kama taasisi kama Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Kiuchumi na Uwekezaji Tanzania (TISEZA), Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) ambazo zote zinatekeleza jukumu la kukusanya watalii.

Marufuku kutisha walipakodi
Sambamba na hayo, amewakemea watumishi wa TRA kutowatisha walipakodi hususani katika kufanya makadirio kwa kuwabambika makadirio makubwa ambayo hayalingani na biashara ya mtu.

“Tujitahidi sisi ni wataalamu, tunapotoa makadirio yetu yawe ni makadirio ambayo sisi wenyewe tunayaamini na hayataleta taswira mbaya kwa taasisi yetu ya mamlaka ya mapato,” alisisitiza.

Ushindani usio halali kwa walipakodi

Waziri wa Fedha ameonya kuhusu ushindani usiokuwa halali kwa walipa kodi unaosababishwa na ukwepaji wa kodi katika maeneo mbalimbali hali inayosababisha upotevu mkubwa wa mapato ya serikali.

“Pamoja na mafanikio mazuri tuliyoyapata katika ukusanyaji wa kodi ndani ya mwezi mmoja (Desemba 2025), bado kuna maeneo kuna ukwepaji mkubwa wa kodi,” aliongeza.

Makusanyo juu miakaminne

Alieleza katika kipindi cha miaka minne mapato yameongezeka kwa asilimia 45 kutoka Sh trilioni 22.2 mwaka 2021/2022 hadi Sh trilioni 32.26 mwaka 2024/25.

Tanzania mfano wa kuigwa Afrika

Aliipongeza TRA kwa kuijengea heshima kubwa Tanzania ndani na nje ya nchi kutokana na weledi na mafanikio makubwa katika ukusanyaji wa mapato.

Alibainisha kuwa kutokana na mafanikio hayo, nchi jirani zimeifanya Tanzania kituo chao cha mafunzo ya namna ya kuimarisha mamlaka zao katika ukusanyaji wa mapato.

Naye Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuph Mwenda alisema mafanikio yaliyofikiwa ni ya Watanzania wote ambao ni wafanyabiashara wakubwa kwa wadogo.

Kuhusu makusanyo ya Desemba 2025 ya Sh trilioni 4.13 yaliyovunja rekodi ya TRA tangu iundwe mwaka 1995, Mwenda alizitaja idara zilizochangia pakubwa kuwa ni Idara ya Walipakodi Wakubwa Sh trilioni 1.914, Idara ya Forodha Sh trilioni 1.286, Idara ya Walipakodi Wadogo na wa Kati Sh bilioni 838 na Kodi za Muungano Sh bilioni 91.6.

Katika kipindi cha Julai hadi Desemba mwaka jana, TRA ilitegemewa kukusanya Sh trilioni 18.1 lakini ilivuka
lengo na kukusanya Sh trilioni 18.77.

Mafanikio hayo yanafunzo gani?
“Ujumbe tunaoupata kutokana na takwimu hizo ni kwamba tunaweza kukusanya kodi kwa kiwango kikubwa tunavyotaka bila kutumia nguvu,” alifafanua Mwenda.

Aliahidi kuwa TRA katika miezi sita iliyobaki katika mwaka huu wa fedha, itaendelea kusimamia utulivu
wa kodi kwa kufanya usimamizi wa kodi kwa wafanyabiashara wa Tanzania.

Matarajio ya miezi sita ijayo

Mwenda alisema TRA itaendelea kuboresha huduma ya ukusanyaji wa kodi kwa kuongeza elimu ya mlipakodi
pamoja na ukusanyaji wa kodi pamoja na kuboresha mifumo ya ukusanyaji wa kodi.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. l Get paid over $110 per hour working from home. l never thought I’d be able to do it but my buddy makes over $21269 a month doing this and she convinced me to try. The possibility with this is endless….

    This is what I do………………………………….. https://Www.Cash54.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com

  3. Google provides awesome remote work opportunities, allowing me to earn $2000-$3000 weekly with just 2-4 hours of daily work. It’s been a game-changer, offering flexibility and reliable income. If you’re seeking a genuine way to earn online, don’t miss this chance. Start today and transform your life!
    .
    More Details For Us →→ http://www.big.income9.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button