TRA yafundwa kuepusha migogoro Katavi

KATAVI: Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Katavi imetakiwa kufanya kazi kwa weledi ili kuondoa changamoto zote zinazoweza kusababisha taharuki katika jamii ikiwemo kukamata ovyo wafanyabiashara, kufunga biashara zao pamoja na kusababisha migomo isiyo ya lazima.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf, alipokuwa mgeni rasmi katika Uzinduzi wa Dawati la Uwezeshaji Biashara Mkoa wa Katavi ambapo amesema hafurahishwi na vitendo hivyo huku akisema matarajio yake ni kuona wafanyabiashara wanafanya kazi katika mazingira rafiki.

Kwa upande wake Kaimu Meneja TRA Mkoa wa Katavi Benward Peter amesema dawati hilo limeanzishwa kwa malengo ya kusaidia na kutatua changamoto zote za wafanyabiashara ikiwemo kuwapatia elimu wafanyabiashara wote watakaonufaika na kitengo hicho.

Awali baadhi ya viongozi wa wafanyabiashara kwa niaba ya wafanyabiashara waliiomba TRA Mkoa huo kutumia lugha nzuri pindi wanapotembelea wafanyabiashara huku wakidai kuwa wanatarajia dawati hilo kuwafikisha katika malengo yaliyotarajiwa.

 

Uzinduzi huo uliambatana na kauli mbiu isemayo “TRA Katavi Inashirikisha, Inasikiliza na Inawezesha”

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button