TRA yakusanya bil 116/- Mtwara

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Mtwara imefanikiwa kukusanya Sh bilioni 116 kwa mwaka fedha 2023/2024.

Hayo yamejiri wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha kilele cha siku ya shukrani kwa mlipa kodi katika mkoa wa mtwara iliyoambatana na utoaji wa tuzo ya walipa kodi bora kwa mwaka fedha 2023/2024, ghafla iliyofanyika katika Manispaa ya Mtwara Mikindani huku lengo likiwa ni pamoja na kutambua umuhimu na mchango wa walipa kodi wote mkoani humo.

Meneja wa Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Mtwara, Maimuna Khatibu amesema makusanyo hayo ya Sh bilioni 116 katika mwaka huo wa fedha 2023/2024 yamevuka lengo la makusanyo ya Sh bilioni 28 sawa na asilimia 410 za utendaji.

Hata hivyo kwa mwaka wa fedha 2024/2025 mamlaka hiyo imejiwekea lengo la kukusanya Sh bilioni 152 ambapo katika miezi sita ya kwanza ya mwaka inayoanzia Julai 2024 mpaka Disemba 2024 imefanikiwa kukusanya Sh bilioni 201 na kufikia ufanisi wa asilimia 132 kwa muda wa miezi sita tu.

‘’Mafanikio haya makubwa ya makusanyo ya kodi ni matokeo ya maamuzi ya serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ya uwekezaji wa fedha nyingi katika upanuzi mkubwa wa bandari yetu ya mtwara hali inayoruhusu bandari kuweza kuhudumia meli kubwa za mizigo kama korosho na makaa ya mawe’’amesema Khatibu

Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara, Wakulima na wenye Viwanda Tanzania (TCCIA) Mkowa wa Mtwara, Kizito Galinoma ameipongeza serikali kwa kuhakikisha wafanyabiashara wanafanya biashara zao kwa uhuru hadi wakaona wanao wajibu mkubwa wa kulipa kodi.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala ameishukuru serikali kwa kuongeza na kuboresha vitendea kazi ikiwemo mifumo ya kurahisisha ulipaji kodi ambayo matokeo yake yanaonekena kwa sasa huku akiwapongeza walipa kodi kwa kulipa kodi kwani kodi nyingi zinazokusanywa zinatoka kwa walipa kodi hao ambao ndiyo msingi wa uchumi wao.

‘’Mafanikio haya yametokana na maamuzi ya Rais wetu ya kuifungua mtwara na kuendeleza kuitumia mipaka yetu na usafirishaji wa mazao mbalimbali kupitia bandari yetu ya mtwara, siyo tu kuwa lango la ukusanyaji wa mapato bali wananchi wetu wanaendelea kupata ajira nyingi rasmi na zisizo rasmi kupitia bandari yetu’’amesema Sawala

Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa amesisitiza suala la matumizi ya mashine za kutolea risiti za kielektroniki (EFD) kwa wauzaji kutoa risiti baada ya kuuza na wanunuzi kudai risiti baada ya kununua bidhaa.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button