TRA yapewa tano ukusanyaji mapato

ARUSHA: Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar, ameipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa ufanisi mkubwa katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali, hatua iliyochangia kuimarika kwa uchumi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Tathmini ya Utendaji Kazi wa TRA kwa Nusu Mwaka wa Fedha 2025/26 uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) Balozi Khamis amesema kuwa TRA ilikusanya shilingi trilioni 18.77 katika kipindi cha Julai hadi Desemba 2025, sawa na asilimia 103.7 ya lengo la trilioni 18.10.
Ameongeza kuwa mwezi Desemba pekee TRA iliweka rekodi kwa kukusanya shilingi trilioni 4.13, kiwango cha juu zaidi tangu kuanzishwa kwake.
Amebainisha kuwa mafanikio hayo yanatokana na sera madhubuti na mageuzi ya mifumo ya ukusanyaji mapato chini ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk Samia Suluhu Hassan, hususan matumizi ya teknolojia za kisasa katika usimamizi wa kodi.

Kwa upande wake, Rais wa Chemba ya Taifa ya Biashara Tanzania (TNCC), Vicent Minja, amesema mazingira wezeshi ya biashara yanahitaji haki na usawa katika ulipaji wa kodi, akitaja sekta isiyo rasmi kuwa changamoto kubwa inayosababisha ushindani usio wa haki.
“Tunaamini wigo wa kodi utaongezeka endapo sekta binafsi itashirikishwa kikamilifu. Ushirikiano wa karibu kati ya Serikali na sekta binafsi utamwezesha mfanyabiashara kufanikiwa na kulipa kodi kwa hiari,” amesema Minja.
Amesisitiza kuwa TNCC iko tayari kushirikiana na TRA kutekeleza Hati ya Makubaliano (MoU) iliyosainiwa, kwa lengo la kupanua wigo wa walipa kodi, kuongeza mapato ya Serikali na kuwezesha upunguzaji wa viwango vya kodi ili kuongeza ushindani wa wafanyabiashara wa Tanzania katika masoko ya kikanda na kimataifa.




Google provides awesome remote work opportunities, allowing me to earn $2000-$3000 weekly with just 2-4 hours of daily work. It’s been a game-changer, offering flexibility and reliable income. If you’re seeking a genuine way to earn online, don’t miss this chance. Start today and transform your life!
.
More Details For Us →→ http://www.big.income9.com
l Get paid over $110 per hour working from home. l never thought I’d be able to do it but my buddy makes over $21269 a month doing this and she convinced me to try. The possibility with this is endless….
This is what I do………………………………….. https://Www.Cash54.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com