Tshisekedi akataa rasimu ya amani

KINSHASA : PENDEKEZO la makubaliano ya amani kati ya Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda, linataka kurejesha udhibiti wa serikali katika maeneo yaliyoko mikononi mwa waasi.

Kwa mujibu wa waraka uliosambazwa na Shirika la Habari la Associated Press, pendekezo hilo lililotolewa na Qatar linaainisha hatua tatu za mchakato wa amani.

Mazungumzo hayo yanatarajiwa kufanyika Doha chini ya upatanishi wa pande zote katika siku chache zijazo.Waziri wa Mambo ya Nje wa Ubelgiji, Maxime Prevot, alisema Rais Félix Tshisekedi hajaridhishwa na rasimu ya makubaliano hayo.

Kwa upande wake, kiongozi wa M23, Bertrand Bisimwa, alisema wanamgambo hao hawawezi kutoa tamko lolote kuhusiana na pendekezo hilo kwa sasa. SOMA: Rasimu ya amani yawasilishwa DRC

DRC imeendelea kukabiliwa na machafuko tangu miaka ya 1990 ambapo makundi ya wanamgambo yamesababisha vifo vya mamilioni ya watu.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button