‘Tukivishe Pete CCM Oktoba 29’ Kairuki

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Kibamba kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Angellah Kairuki amesema kwa kazi kubwa iliyofanywa na mgombea urais wa chama hicho Dk Samia Suluhu Hassan katika jimbo hilo anastahili kuvishwa pete ya pongezi ifikapo oktoba 29 kwa kukipigia kura za ndio chama hicho.
Akizungumza wakati wa kampeni zake jijini Dar es Salaam katika kata ya Kwembe Kairuki amesema wananchi hao wanapaswa kupiga kura za ndio ili kupata mafanikio zaidi. “Walisema chanda chema huvishwa pete tukakivishe pete chama cha mapinduzi, tukamvishe pete mama yetu Dk Samia Suluhu Hassan kwakumpatia kura nyingi za kishindo ili na mimi nikiwa nyuma yake kumsaidia kuwa mbunge kwa jimbo la kibamba lakini msimsahau Mgombe diwani wa Kwembe,Haji konde.
Ameongeza “Ndugu zangu ccm tukivishe pete tarehe 29 mwezi wa 10 kwa kukipa kura nyingi naomba msituangushe ndugu zangu safari hii mmepata bahati karatasi ya kura kwa mara ya kwanza mnapata wagombea wawili wanawake lakini na mdogo wetu mwenye jinsia ya kiume naomba msikiangushe ndugu zangu tuchague mafiga matatu.
Amesema serikali imefanya mambo makubwa ambayo ni pamoja na kuweka maktaba katika shule ya msingi ya Kwembe iliyogharimu shilingi milioni 10,ujenzi madarasa uliogharimu sh milioni 40 katika shule ya msingi ya Kwembe na kusaidia wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu .
Amesema serikali ya CCM imewekeza zaidi ya sh bilioni 6. 6 kwa elimu ya sekondari lakini sambamba na hilo imewekeza sh bilioni 5. 8 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Dar es salaam girls ambayo iko katika kata hiyo. “Shule ya sekondari ya King’azi walimu wamejengewa nyumba,tuliweza kununua samani katika shule ya Dar es salaam kwa takriban shilingi milioni 100. 8 ili kuhakikisha inakuwa na mandhari nzuri na watoto wetu hawa wasikae chini.
Kwa upande wa barabara amesema waliwekeza katika matengenezo ya barabara ya st Joseph millenia na Kwembe. Kairuki amesema katika eneo la afya waliweza kuwekeza katika kuboresha zahanati ya Amani kwa gharama zisizo pungua sh milioni 580 na kununua dawa na vifaa tiba uhakika wa upatikanaji wa dawa kwa zaidi ya 98%.
Kwa upande wa uwezeshaji wananchi kiuchumi ameeleza kuwa wametumia sh milioni 32. 1 kwa ajili ya kukopesha kwa makundi maalum yenye uhitaji makundi 26 wakiwemo wanawake ,vijana pamoja na watu wenye ulemavu.
“pande wa maji mtandao wa usambazaji wa maji umejengwa kupitia mradi wa usambazaji wa maji kwa Dar es salaam linaendelea pia katika kata yetu ya kwembe lakini sambamba na hilo tunalo mradi kwa kingazi B kwa ajili ya kuongeza msukumo wa maji na swala hili limefanyika vizuri na kupitia ujenzi wa tenki yetu ya Bangulo ambao kwa sasa unaendelea na majaribio tunaamini utaongeza sana upatikanaji wa maji kiwango cha juu cha upatikanaji wa maji Kwembe ni asilimia 95.
Amesema kwa upande wa wa king’azi tumeendelea kuboresha mradi wetu wa maji kwa kutumia shilingi milioni 33. 3 na tayari wateja wamenufaika 3, 154 na kazi inaendelea. “Lakini tunaendelea pia kuwekeza katika miradi midogo ya upanuzi wa maji tumetekeleza Malamba mradi wa sh milioni 157, mradi wa kwembe babu Sh milioni 66. 9 na wanufaika 1995 tayari wanapata maji. SOMA: Samia: Vijana lindeni amani
Medical debt had me stressed, but this online approach has been a blessing. I now earn about $7,700 monthly. Details >>>> https://dailycash21.blogspot.com/