Tume kuchunguza vurugu Oktoba 29

DODOMA: RAIS, Dk ๐ฆ๐ฎ๐บ๐ถ๐ฎ ๐ฆ๐๐น๐๐ต๐ ๐๐ฎ๐๐๐ฎ๐ป amesema Serikali imeunda tume ya kuchunguza vurugu zilizotokea nchini Oktoba 29 wakati wa Uchaguzi Mkuu, ili kujua kiini cha tatizo hilo, akieleza kuwa taarifa hiyo itaongoza kujielekeza kwenye mazungumzo ya kuleta maelewano na amani.
Dk Samia ametoa kauli hiyo leo Novemba 14, 2025 wakati akifungua bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo aliwataka wabunge na wageni waalikwa bungeni kusimama kwa dakika moja kwa ajili ya kuwaombea waliopoteza maisha kwenye vurugu zilizotokea siku hiyo.
Ametoa pole kwa waliopoteza ndugu zao, kujeruhiwa na kupoteza mali na kusema tume hiyo itasaidia kufahamu chanzo cha machafuko hayo na kufahamu ni wapi pa kuanzia katika kuijenga Tanzania yenye umoja na amani kama ilivyozoeleka.
โBinafsi nimehuzunishwa sana na tukio lile natoa pole kwa familia zote zilizopoteza wapendwa wao tunaomba waliofariki wapumzishwe kwa amani, kwa majeruhi tunawaombea wapone haraka na waliopoteza mali zao tunawaomba wawe na ustahimilivuโ amesema Dk Samia na kuongeza kuwa
Ni vyema Watanzania wakarejea kwenye msingi wa amani iliyozoeleka kwani ndio utambulisho wa Tanzania huku akiahidi kutekeleza yote aliyoyaahidi kipindi cha kampeni za Uchaguzi Mkuu.



