Tume utumishi wa mahakama yatakiwa kusimamia maadili

WATUMISHI wa Tume ya Utumishi wa Mahakama wameagizwa kubaini na kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazotokana na uhalisia wa bajeti husika ikiwemo kuweka mikakati ya utoaji elimu za kimaadili kwa maofisa mahakama ngazi ya mikoa na wilaya nchini.

Aidha Tume ya Utumishi imepongezwa kwa kuzingatia stahiki za watumishi ikiwemo kusimamia maadili ya utumishi pamoja na utunzaji wa siri haswa katika taarifa za mahakimu.

Advertisement

Hayo yalisemwa leo Jijini Arusha na Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Arusha, Ilvin Mugeta wakati wa kufungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Utumishi wa Mahakama sambamba na kujadili taarifa ya utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2025.

Amesema ni vema kuimairisha kamati za maadili kwa watumishi wote kwa kuwajengea uwezo wa kifedha na kiujuzi watumishi wa tume hiyo pamoja na utoaji elimu kwa kamati za maadili za mahakama ili kuziimarisha zaidi.

“Tume ya Utumishi wa mahakama angalieni mbinu ya kuimarisha utendaji wa kusimamia kamati za uongozi za mahakama lakini pia nawapongeza kwa matumizi sahihi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ambapo awali maombi ya kazi yalikuwa yakitumiwa kupitia karatasi lakini sasa maombi hayo yanafanyika kupitia Tehama,”.