Tunaitambua Palestina – Keir Starmer

LONDON: UINGEREZA , Australia na Canada zimetangaza kulitambua rasmi taifa la Palestina, hatua inayotajwa kuwa mabadiliko makubwa ya sera za kigeni za mataifa ya Magharibi na imechochea hasira kutoka Israel.

Tangazo hilo limekuja wakati Israel ikikabiliwa na shinikizo kubwa la kimataifa kuhusu vita vya Gaza vilivyochochewa na shambulizi la Hamas Oktoba 7, 2023. SOMA: Australia yatangaza kuitambua Palestina

Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer, kupitia ukurasa wa X alisema hatua hiyo inalenga kufufua matumaini ya amani kwa Wapalestina na Waisraeli kupitia suluhisho la mataifa mawili. Uingereza na Canada zimekuwa nchi za kwanza za G7 kuchukua hatua hiyo huku Ufaransa ikitarajiwa kufuata.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button