Tupambane na ‘mtoto wa jicho’ kuyalinda maisha ya Mtanzania

TAKWIMU zinaonesha mtoto wa jicho ni miongoni mwa changamoto kubwa za kiafya nchini, na husababisha takribani asilimia 20 ya upofu Tanzania.
Mkuu wa Idara ya Macho Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk Joachim Kilemile akihitimisha kambi ya matibabu hayo anasema kati ya wagonjwa 24 wanaofika hospitalini wakiwa vipofu, 19 kati yao hukutwa na tatizo hilo, jambo linaloonesha ukubwa wa hitaji la huduma za matibabu ya mtoto wa jicho.
Ni wazi takwimu hizi zinatukumbusha ukweli usiopendeza lakini wenye uhalisia mkubwa ndani yake kwa sababu Watanzania wengi wanaendelea kuishi gizani, si kwa ukosefu wa nuru, bali kwa upofu unaosababishwa na tatizo linaloweza kutibika kwa mkono wa mtaalamu.
Mgonjwa anaweza kuona tena baada ya upasuaji wenye muda mfupi, maumivu madogo, na matokeo ya uhakika. Nionavyo mimi suala la matibabu linatupa picha mara mbili moja ni ukubwa wa kisayansi wa hatua zilizofikiwa, na wakati huohuo, ukubwa wa mapungufu tuliyonayo kama taifa kwenye upatikanaji wa huduma za macho.
Taarifa za wagonjwa 60 kufanyiwa upasuaji wa mtoto wa jicho kwa njia ya tundu dogo MNH kwa kushirikiana na Vision Care ya Korea Kusini, zinatoa matumaini makubwa kwa mtu ambaye amepoteza uoni, kurudishiwa uwezo wa kuona si tu kubadilishiwa hali ya kiafya, bali ni kupewa maisha mapya.
Anayeweza kuona tena anaweza kurudi kazini, kuwatunza watoto wake, kushiriki kikamilifu katika shughuli za jamii, na kuondokana na utegemezi usio wa lazima na kwa lugha rahisi, upasuaji huu si tiba tu bali ni ukombozi wa kijamii, kiuchumi na kisaikolojia.
Lakini wakati tunapongeza hatua na mafanikio hayo, hatuwezi kufumbia macho ukweli kwamba wagonjwa 60 ni sehemu ndogo ya wengi wenye tatizo nchini. SOMA: 1,499 wakutwa na matatizo ya macho mikoa miwili
Hii ina maana kuwa asilimia 79 ya upofu unaotibiwa hospitalini unatokana na tatizo hilo pekee. Tunahitaji mpango maalumu wa kitaifa kama ilivyo kwa Ukimwi, Kifua Kikuu au malaria. Kutibu macho si anasa bali ni uwekezaji katika nguvu kazi ya taifa kwani hakuna maendeleo bila watu wenye uwezo wa kuona. Tunapoacha wazee, wakulima, wafanyabiashara wadogo, au walimu kupoteza uoni kwa tatizo linalotibika, tunalinyima taifa nguvu kazi iliyoko mikononi mwao.
Uwekezaji katika macho ni uwekezaji katika uzalishaji wa taifa. Pia, ushirikiano wa kimataifa kama huu kati ya MNH na Vision Care ya Korea Kusini unapaswa kupewa nguvu kwa kuwekwa mikakati ya kuongeza ujenzi wa uwezo wa misaada na wataalamu wa nje, tunapaswa kuhakikisha matabibu wa ndani wanapewa mafunzo ya hali ya juu, vifaa vinapatikana kwa kudumu, na hospitali zinakuwa na uwezo wa kujitegemea baada ya muda.
Ushirikiano na wadau wa nje uwe njia ya kutujengea uwezo, si kutufanya wategemezi wa milele. Natamani zifanyike kampeni za kitaifa za uhamasishaji kupitia vyombo vya habari, serikali za mitaa na taasisi za dini ili kuondoa hofu na imani potofu kwa jamii na itambue kuwa kuishi gizani kunatibika, na kila mmoja ana haki ya kuona tena.
Sisi Watanzania tuwe tayari kuwaona matabibu mapema tunapopata shida za kiafya hasa macho kwani hatupaswi kuwa vipofu kwa sababu ya ugonjwa unaotibika hivyo utayari, sera, uwekezaji na dhamira ya muda mrefu viwezeshe hili.




JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com
Google provides awesome remote work opportunities, allowing me to earn $2000-$3000 weekly with just 2-4 hours of daily work. It’s been a game-changer, offering flexibility and reliable income. If you’re seeking a genuine way to earn online, don’t miss this chance. Start today and transform your life!
.
More Details For Us →→ http://www.big.income9.com