Tusipoamka tutaendelea kushangilia mafanikio ya kina Pacome

TUTAENDELEA kumshangilia Pacome Zouzoua akiwa sehemu ya kikosi cha Ivory Coast kilichofuzu tena fainali za Kombe la Dunia, tangu mwaka 2014 iliposhiriki kwa mara ya mwisho Brazil.
Ni miaka 11 imepita tangu taifa hilo kubwa kwenye mchezo wa mpira wa miguu Afrika kufuzu fainali za Kombe la Dunia lakini kwa Tanzania bado tumekuwa tukiota ndoto za mchana kwamba pengine siku moja tutafuzu.
Cape Verde yenye watu wasiofika 600,000 imeweka historia ya kuwa moja ya mataifa madogo kwenye mpira wa miguu kufuzu fainali hizo ikiungana na Togo na Angola zilizowahi kufanya hivyo kwenye fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika Ujerumani mwaka 2006.
Tanzania yenye watu zaidi ya milioni 60 bado tunapambana kuona siku moja na sisi tunakuwa sehemu ya mafanikio hayo ambayo Togo, Angola na safari hii Cape Verde wameyapata. Ni vizuri kuwa na ndoto za kufuzu fainali hizi kwani mafanikio yoyote yanaanza na kutamani lakini ndoto zisizokuwa na mipango madhubuti ndizo hizi zinaitwa ndoto za mchana ambazo mara nyingi hazina uhalisia wowote.
Lakini inawezekana kabisa kuota ndoto zitakazokuja kuwa na mafanikio kama ndoto hizi zitaambatana na mipango ya kitaalamu ya kuzifikia, siyo kama hizi ambazo hamasa, shauku na matamanio yametawala au yamezidi mipango ya kitaalamu.
Ni sawa na kutamani kwenda peponi huku ukiogopa kifo na wakati unajua fika namna pekee ya kwenda peponi ni lazima ufe kwanza. Au ni sawa na kuwa na majibu rahisi kwenye maswali magumu; tunakabiliwa na maswali magumu lakini tunatoa majibu mepesi kwenye kujibu maswali hayo, sio rahisi kufika tunapotaka kwenda.
Hatuna mipango ya kitaalamu ya kuinua mpira wetu au ya kutengeneza wachezaji na makocha wenye uwezo mkubwa watakaokuja kuibua vipaji kwenye taifa hili lenye watu zaidi ya milioni 60.
Tunatoa majibu mepesi tu kuanzia ujenzi wa timu zetu kwamba zikitaka kushindana basi ni lazima kwenda mataifa ya Magharibi mwa Afrika kusajili wachezaji wenye uwezo mkubwa huku tukishindwa kuandaa vijana watakaowapa maswali magumu nyota hawa wa kigeni.
Kwa mtindo huu tutaendelea tu kushangilia mafanikio ya kina Pacome tukiamini ni yetu kwa sababu wanacheza kwenye ligi ya Tanzania lakini kiuhalisia siyo. Kama ambavyo tumewahi kushangilia mafanikio ya Nonda Shaabani miaka mingi nyuma tukiamini ni mafanikio yetu kwa sababu aliwahi kuwa mchezaji wa Yanga.
Nonda Shaabani aliyeichezea Yanga katikati ya miaka ya 1990 kabla ya kwenda Afrika Kusini na baadaye FC Zurich ya Uswisi, Monaco ya Ufaransa na klabu mbalimbali za Ulaya alikuwa hakauki kwenye midomo yetu tukiamini anachofanikiwa huko Ulaya ni chetu kwa sababu alipita Yanga.
Akawa mmoja wa wafungaji bora wa muda wote na nahodha wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kwenye miaka yake ya ubora lakini bado tulikuwa tunajivunia mafanikio yake tukiamini ni yetu.
Ili tuwe na mafanikio yetu ni lazima tuzalishe wachezaji wetu kuanzia ngazi ya watoto watakaokuwa na misingi mizuri ya mpira wa miguu itakayowafanya watambe kwenye klabu mbalimbali za Ulaya na kuiletea mafanikio Taifa Stars.
Ili kufanikisha, hakuna njia ya mkato lazima tukubali kuwekeza hasa kwa maana ya kupeleka makocha wazawa kwenye vyuo mbalimbali vya ukocha vya Ulaya na mataifa mengine yaliyopiga hatua kubwa katika mchezo huu.
Miaka ya nyuma kwa maana ya miaka ya 1970, kulikuwa na makocha ambao walipelekwa Ulaya na nchi mbalimbali zilizopiga hatua kubwa kwenye mchezo wa soka kama vile Abdallah Kibadeni, Charles Boniface Mkwasa, Dr Mshindo Msolla, marehemu Syllersaid Mziray, Rogatian Kaijage, marehemu Paul West Gwivaha, marehemu Mansour Magram na wengineo ambao waliporudi walizalisha nyota wengi wa maana.
Lakini katika mpango huo wa kuandaa timu kutoka ngazi ya watoto, waletwe makocha waliosoma programu hizo za watoto maana sio kila kocha wa mpira wa miguu ni mzuri kwenye kufundisha watoto; waletwe makocha wa kila hatua, wa watoto, vijana na wakubwa mbali na wazawa watakaopelekwa nje kusoma.
Nje ya hatua hizi ni ngumu kama taifa kupiga hatua tunazotamani kwenye mchezo wa soka.
I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com