Uchaguzi Mkuu Malawi kufanyika leo

LILONGWE , MALAWI : WANANCHI wa Malawi leo wanapiga kura kuchagua viongozi wa ngazi ya urais, ubunge na udiwani katika uchaguzi unaoelezwa kuwa na ushindani mkali.

Uamuzi wa wapigakura unatarajiwa kumweka madarakani kiongozi atakayekabiliana na changamoto zinazolikabili taifa hilo la kusini mwa Afrika, zikiwemo mfumuko wa bei na uhaba wa nishati ya mafuta, masuala yanayowapa hofu na changamoto kubwa wananchi.

Kiti cha urais kinawaniwa na wagombea 15 akiwemo Rais wa zamani, Joyce Banda, lakini ushindani mkali unatabiriwa kuwa kati ya Rais Lazarus Chakwera na mtangulizi wake, Peter Mutharika. Chakwera aliingia madarakani mwaka 2020 baada ya kuishutumu serikali ya Mutharika kwa vitendo vya ufisadi. Hata hivyo, utawala wake nao umekumbwa na tuhuma za rushwa pamoja na kudorora kwa uchumi.

Mbali na kinyang’anyiro cha urais, wapigakura wapatao milioni 22 wanashiriki pia katika kuwachagua wabunge na madiwani. SOMA: Biashara Tanzania, Malawi sasa ioneshe ‘sura mpya’

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button