UDP yaahidi viwanda kila mkoa

MOROGORO: MGOMBEA urais wa Chama cha United Democratic Party (UDP), Saum Rashid, ameahidi kuwa endapo atapata ridhaa ya wananchi kumchangua kuwa Rais, serikali yake itajenga kiwanda kila mkoa kulingana na rasilimali zilizopo ili kuinua uchumi wa wananchi na kuzalisha ajira kwa watanzania .

Saum ameyasema hayo kwenye mkutano wa kampeni za chama hicho kunadi sera zake uliofanyika katika eneo la soko la Mji Mpya , kata ya Mji Mpya , Manispaa ya Morogoro Septemba 28,2025.

Amesema Serikali ya UDP endapo itaingia madarakani, itatekeleza vipaumbele vikuu vitano vilivyopo katika Ilani ya Uchaguzi ambavyo ni uboreshaji wa miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji ,ujenzi wa viwanda, uboreshaji huduma za afya ,elimu na maji.

Saum amesema katika suala la viwanda, Serikali yao imedhamiria kujenga viwanda katika mikoa yote ya Tanzania kulingana na rasilimali zilizopo kwenye mkoa husika.

 

“Kama tunavyojua Mkoa wa Morogoro ni mkoa wa viwanda, lazima turudishe uwekezaji huu ili uweze kuwasaidia wananchi na lengo kubwa ikiwa ni kufungua fursa za ajira, kukuza uchumi wa watanzania wote na kukuza uchumi wa taifa letu,” amesema .

“Tukiwa na viwanda hapa Morogoro kwa maana wataajiriwa watoto wetu, tutapunguza uhaba wa ajira ,utafungua soko kwa mazao mbalimbali ,hatutauza malighafi na badala yake mazao yataboreshwa kwa kuchakatwa na bidhaa zitauzwa kwa bei kubwa na zenye ubora kwa ajili ya watanzania na kuuzwa nje ya nchi,” amebainisha Saum.

Mgombea urais huyo amesema ukijenga viwanda vingi kuna changiakukuza uchumi na hivyo kuondokana na utengemezi , kujikomboa kiuchumi baada ya kuweka misingi imara na thabiti.

“ Serikali yetu itakayoongozwa UDP, tumejinasibu, tumefanya utafiti wa haya na yanawezekana, yanatekelezeka , tunaomba ridhaa yenu wananchi Oktoba 29, 2025 mtupikie kura na kutuchagua tuongoze Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili mabadiliko haya ya kiuchumi yaweze kuwasaidia watanzania wote na hasa wanyonge” amesema

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button