Sekta ya nguruwe kupata msukumo mpya

DAR-ES-SALAAM : WAZIRI Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda, amesema Tanzania itanufaika na kongamano kubwa la wafugaji wa nguruwe Barani Afrika, litakalosaidia kufungua fursa za uwekezaji, kuongeza wigo wa bidhaa za nguruwe, kuimarisha uhusiano wa wafugaji, kubadilishana uzoefu na kukuza soko kitaifa na kimataifa.

Akizungumza jana wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo linalofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Septemba 11 hadi 13, 2025, Pinda alisema pamoja na fursa, lengo ni kutatua changamoto zinazoikabili sekta hiyo kupitia mafunzo, vipindi vya uwasilishaji, mijadala ya kibiashara na ziara za viwandani.

“Watajadili pia fursa za kimkakati kama matumizi ya teknolojia na masoko ya nje. Ufugaji wa nguruwe unazalisha maelfu ya ajira na protini, na unaendana na malengo ya taifa ya kukuza uchumi, kuboresha maisha ya wakulima na kuongeza thamani ya bidhaa,” alisema.

Alibainisha changamoto kuu zinazokabili sekta hiyo kuwa ni uhaba wa mifugo bora, gharama kubwa za chakula, kukosekana kwa bei elekezi, magonjwa kama homa ya nguruwe na ukosefu wa bima ya mifugo. SOMA: Mapafu ya nguruwe kupandikizwa binadamu

Pinda alipendekeza hatua za kudhibiti changamoto hizo ikiwemo kuanzishwa kwa vituo vya kikanda vya kuzaliana, kushirikiana na taasisi za utafiti, kuweka ruzuku ya malisho, kupunguza kodi kwenye viambata vya chakula na kuandaa mpango wa kitaifa wa kufuatilia magonjwa ya nguruwe.

Habari Zifananazo

7 Comments

  1. I just got paid $22k working off my laptop this month!** And if you think that’s cool, my divorced friend has twin toddlers and made over $22620 her first month.details on this website**Want the secret?** Copy this Website and choose HOME TECH OR MEDIA……..

    Here is I started_______ https://Www.Jobathome1.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button