UJUMBE KUELEKEA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 29/2025

KUELEKEA uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29 mwaka huu, kijana Joshua Atanazi ametoa ujumbe wake amewataka vijana na wananchi kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi la kupiga kura ili kuchagua viongozi bora watakaowaletea maendeleo

Akizungumza na vijana wenzake, Atanazi amesema kundi la vijana lina idadi kubwa nchini na ndiyo lenye nafasi ya kufanya mabadiliko chanya kupitia kura zao. “Kwa sababu sisi vijana ndiyo wengi sana hivi sasa, na huu ndiyo muda wetu wa kuamua kwa kupiga kura, Ni muhimu tumchague kiongozi bora atakayetunga sera nzuri. Usipopiga kura, kesho usilalamike kwamba kiongozi hakufanyii kazi, ilhali hukushiriki kumchagua,” ameema Atanazi. SOMA: CCM yaongoza kwa uzoefu-Dk.Nchimbi

Asema jukumu la kila Mtanzania, hususan vijana, ni kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi ili kupata viongozi watakaoongoza taifa kwa haki na uwajibikaji. “Hivyo basi vijana, wazee na kina mama, tushirikiane kupiga kura ifikapo tarehe 29, ili tuwapate viongozi bora watakaoongoza nchi kwa manufaa ya wote,” alisema kwa msisitizo.

Kwa mujibu wa Atanazi, kujitokeza kupiga kura ni hatua muhimu ya kutimiza wajibu wa kiraia na msingi wa kuwa na haki ya kuwawajibisha viongozi baada ya uchaguzi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button