Ukitupa taka hovyo faini mil 1/-

MKUU wa Mkoa wa Arusha, Paulo Mkonda,amesema kuanzia Desemba Mosi mwaka huu, mwanachi yoyote atakayetupa taka hovyo atatozwa faini ya Sh milioni 1, lengo kuimarisha usafi wa jiji la Arusha.

Makonda amesema hayo leo jijini humo Arusha mara baada ya kuzindua kampeni ya usafi katika soko la Kilombero, kata ya Levolosi.

Advertisement

Amesema Halmashauri ya Jiji la Arusha imeingia mkataba na Suma JKT ya kuhakikisha inawadhibiti watu wanaochafua mazingira.

Amesema tabia ya usafi haibadilishwi kwa kuchekeana hivyo Suma JKT watasimamia hilo ,akawataka wenye maduka kuhakikisha maeneo yo yanakuwa safi, pia amewaonya mama lishe wanaomwaga maji hovyo ya kuoshea vyombo vyao barabarani kuacha mara moja.

Pia Suma JKT imepewa jukumu lingine kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola kuwakamata vibaka na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano .