Umoja wa Afrika wampongeza Mutharika kwa ushindi

ETHIOPIA : UMOJA wa Afrika umempongeza Peter Mutharika kwa kushinda uchaguzi nchini Malawi. Pia wametoa pongezi kwa wananchi wa taifa hilo kwa kushiriki kampeni za amani na mchakato wa kidemokrasia kwa utulivu.

Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Umoja huo, Mahmoud Ali Youssouf, ameyasema hayo kupitia mtandao wa X. SOMA: Mutharika ashinda uchaguzi Malawi

Mutharika, aliyekuwa madarakani kati ya mwaka 2014 na 2020, ameshinda tena kwa kupata asilimia 57 ya kura. Rais anayeondoka, Lazarus Chakwera, alipata asilimia 33, kulingana na Tume ya Uchaguzi ya Malawi iliyotangaza matokeo ya uchaguzi.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Annabel Ntalimanja, amesema: “Sisi sote ni Wamalawi na tuko imara zaidi ya vyote vinavyotutenganisha. Tushirikiane kuitumikia nchi yetu na kuviandalia vizazi vijavyo Malawi iliyo bora, imara na yenye mafanikio.”

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button