Unachohitaji kujua kuhusu bima yako ya afya

BIMA ya afya sio tena anasa bali ni lazima. Pamoja na gharama za matibabu zinazoongezeka, mpango Bima sahihi na unaofaa unatoa ufikiaji wa huduma muhimu bila mzigo wa msongo wa kifedha.

Hata hivyo, wengi hupata kujua mapungufu ya mipango bima yao wanapokutana na bili ya hospitali.

Si mipango yote ya bima ya afya ni sawa. Baadhi hujumuisha matibabu ya kutwa, lakini hazijumuishi ushauri wa wataalamu, wakati mwingine hujumuisha huduma za uzazi au usimamizi wa magonjwa sugu.

Ingawa katika uchaguzi wa mpango bima sahihi, kampuni za bima ya afya zimefanya kuwa matibabu ya kulazwa iwe ni lazima.

Ni muhimu kujua wazi nini kilicho kwenye mpango wako wa bima. Je, unahusisha uchunguzi wa kawaida? Vipi kuhusu dharura? Kuelewa maelezo haya kutakusaidia kufanya maamuzi sahihi kuhusu afya yako.

Gharama ni jambo muhimu

Licha ya mpango bima kuwa na gharama nafuu, inapaswa kuangalia je inakuja na mafao ya aina gani?

Unaweza kujikuta kuwa unalipia gharama nafuu lakini mafao utakayopata ni machache kwa hiyo haitaendana na matakwa yako kama wewe ulikuwa ukihitaji mafao kama vile ya uzazi, macho, meno, matibabu ya kutwa na kulazwa.

Unaweza kujikuta ukilipa zaidi unapotafuta matibabu. Kupata uwiano mzuri kati ya gharama nafuu na mpango kamili ni muhimu.

Kwa mfano, Bima ya Afya ya Jubilee inatoa mipango maalum ya afya inayotoa mipango bima ya kuaminika kwa watu binafsi, familia na kampuni.

Rogation Selengia

 

Iwe unahitaji huduma ya matibabu ya kutwa, kulazwa, matibabu maalum, au manufaa ya ustawi, mipango yetu imetengenezwa kukulinda kutokana na gharama zisizotarajiwa za matibabu.

Washauri wa kifedha wa kampuni hiyo husaidia watu kila hatua, kuhakikisha wanachagua mpango bora kwa mahitaji yao. Ukiwa na mpango bima sahihi, unaweza kupata huduma ya afya yenye ubora kwa kujiamini.

Pitia bima yako ya afya leo ili kuelewa chaguzi zinazopatikana na kuhakikisha mpango wako una kile kinachohitajika zaidi.

Linapokuja suala la afya yako, hakuna nafasi ya kudhania, bali kuwa na taarifa na kuwa tayari ni muhimu ili kukabiliana na maisha kwa amani na afya bora ya akili.

*Mwandishi ni Ofisa Mkuu wa Usambazaji, Jubilee Health Insurance

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button