Upande wa mashitaka wakwama ushahidi kesi wanandoa

UPANDE wa mashitaka katika kesi ya shambulio la mwili na lugha ya matusi inayowakabili wanandoa Bharat Nathwan na mkewe Sangita Bharat umeshindwa kuendelea kutoa ushahidi wake.

Hayo yalidaiwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Beda Nyaki.

Wakili wa Serikali, Frank Rimoy alidai kwa kuwa hakimu anayeisikiliza kesi hiyo hayupo hivyo usikilizwaji hautaendelea.

Advertisement

“Kesi hii huwa inasikilizwa na hakimu Lyamuya, kwa kuwa mheshimiwa hayupo, tunaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kusikilizwa,” alidai Rimoy.

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka, Julai 21, 2023, Bharat Nathwan na mkewe Sangita walimshambulia Kiran Lalit na mkewe kwa kumtumbukiza Kiran kwenye ndoo ya saruji iliyochanganywa na kumtolea lugha ya matusi mke wa Lalit.