Usalama wavutia wawekezaji Kigoma

KIGOMA: MAZINGIRA mazuri ya uwekezaji, amani na usalama mkoani Kigoma ambavyo vimesimamiwa kwa karibu na serikali vinaelezwa kuwa chachu kubwa ya kuwafanya wawekezaji kwenye sekta mbalimbaali kujitokeza na kuwekeza mkoani Kigoma.
Meneja wa Shule ya Awali na Msingi ya Ndameze iliyopo mkoani Kigoma, Method Kokoe amesema hayo wakati wa mahafali ya nane ya darasa la saba ya shule hiyo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita na kusema kuwa kwa sasa mazingira yaliyowekwa na serikali yamefanya kuwe na maendeleo makubwa na kuvutia idadi kubwa ya wawekezaji.
Kokoe amesema hali hiyo imefanya shule hiyo kupanua huduma zake na kuongeza shule ya sekondari ambayo itaanza mwezi Januari mwakani na kwamba mazingira hayo yamefanya pia shughuli za biashara na uchumi kufanyika kwa tija hivyo wazazi wengi kuweza kusomesha watoto wao kwenye shule za mchepuo wa Kingereza.
Msanii wa Muzikiwa Bongo Fleva, Clayton Chipando maarufu Baba Levo ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya nane ya Shule ya Awali na Msingi ya Ndameze akikabidhi cheti cha kuhitimu kwa mwanafunzi Veneranda Isaya (kulia) mwanafunzi aliyeongoza kwa kufanya vizuri kwenye somo la hesabu katika shule hiyo.
Amesema Shule ya Msingi Ndameze amewatoa hofu watu wote kwamba Mkoa Kigoma ni salama tofauti na hali ya vita iliyopo kwa nchii jirani na kwamba shule hiyo kwa uwekezaji wake imekuwa kufanya vizuri kitaaluma kwa mwaka jana kushika nafasi ya nane kitaifa na kuongeza idadi ya wanafunzi kila mwaka.
Wahitimu wa darasa la saba katika Shule ya Awali na Msingi Ndameze wakiwa Katika mahafali shuleni hapo
Akizungumza katika mahafali hayo, Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Clayton Chipando maarufu ‘Baba Levo’ ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali hayo alisema kuwa mazingira mazuri na hali ya usalama ndiyo inayochangia watu wengi kuwekeza mabilioni ya shilingi kwenye miradi mbalimbali mkoani Kigoma ikiwemo uwekezaji mkubwa wa shule hiyo.
Baba Levo ambaye ni mgombe ubunge Jimbo la Kigoma Mjini amesema kuwa mmiliki wa shule hiyo, Salvaroty Chobaliko mbali na kuwekeza kwenye shule hiyo pia amewekeza kwenye hotel ya nyota nne ya Sunset Vista na kutoa ajira kwa idadi kubwa ya wananchi wa mkoa Kigoma hivyo akaomba mwekezaji huyo kuungwa mkono kwawazazi kupeleka watoto wao shule hapo.
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com