Uturuki waipa Muhas gari ya wagonjwa

SERIKALI ya Uturuki chini ya Shirika la Maendeleo la Uturuki (TIKA) lililopo Tanzania limetoa gari la kubebea wagonjwa ‘ambulance’ kwa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) yenye lengo la kukuza sekta ya afya nchini.

Akizungumza leo Machi 5, 2025 jijini Dar es Salaam mara baada ya kukabidhiwa gari hilo, Makamu Mkuu wa MUHAS, Profesa Appolinary Kamuhabwa amesema hatua hiyo imechangiwa na ushirikiano mzuri baina ya chuo na serikali ya Uturuki.

Prof Kamuhabwa amesema ushirikiano baina yao imewasaidia pia katika hospitali yao ya kinywa na meno hivyo baada ya kukabidhiwa gari hilo litaenda kusaidia kwenye kitengo cha magonjwa ya dharura.

Kwa upande wake Dk Said Kilindimo Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali kutoka MUHAS amesema gari hilo litasaidia kufundishia wanafunzi kutokana na magonjwa ya dharura kwani sasa hivi magonjwa ya dharura yamekuwa mengi.

Rais wa TIKA, Bekir Gezer amesema uturuki katika kukuza sekta ya afya duniani wamefanya miradi mbalimbali hivyo na leo wapo katika taasisi muhimu kwa nchi ya Tanzania na watakuza ushirikiano vyema.

Katika hatua nyingine TIKA imetembelea jengo la watoto ambalo wamefanya ukarabati katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili pamoja na viwanda vidogo vya wajasiriamali vilivyopo Mwananyamala .

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button