Uwepo pembejeo waongeza uzalishaji korosho

MTWARA: UWEPO wa pembejeo za ruzuku katika zao la korosho na kuongezeka kwa tija ya uzalishaji kumeleta manufaa makubwa kwa wakulima wa zao hilo nchini hasa ongezeko la kipato.
Akizungumza mkoani Mtwara, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) Francis Alfred amesema kabla ya serikali ya awamu ya sita kuingia madarakani wahakuwa na ruzuku katika zao hilo kwani wakulima walikuwa wakijitegemea kununua pambejeo kwa fedha zao wenyewe.
‘’Kipindi hicho bei ya korosho wala haikuwa mzuri sana wakulima walikuwa wanahangaika kipato wanachokipata wao ndiyo wanaenda kununua pembejeo lakini kuanzia mwaka 2021/2022 serikali ya awamu sita ilianzisha ruzuku ya pembejeo kwa wakulima,” amesema Francis.
Uwepo wa serikali hiyo madarakani imeweza kutoa pembejeo za ruzuku za zao hilo katika misimu mbalimbali ya kilimo ikiwemo mwaka 2021/2022 ambapo ilitoa pembejeo zenye thamani ya Sh bilioni 59.4.
Pia mwaka 2022/2023 ilitoa pembejeo za Sh bilioni 96.3, mwaka 2023/2024 pembejeo za Sh bilioni 189.3 na mwaka 2024/2025 pembejeo za Sh bilioni 281.
Matokeo ya pembejeo hizo wanajionea uzalishaji wa korosho umekuwa ukiongezeka kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo ikiwemo mwaka 2022/2023 ulizalishaji ulikuwa ni zaidi ya tani 100,000, 2023/2024 uzalishaji ukuwa ni zaidi ya tani 300,000 na mwaka 2024/2025 uzalishaji ulikuwa ni zaidi ya tani 500,000.
Jitihada zingnine zinazofanywa na serikali katika zao hilo ikiwemo utafutaji wa wanunuzi na masoko ya korosho ambapo msimu uliyopita mwaka 2024/2025 bei ya korosho iliongezeka kufikia wastani wa Sh 3,592 kwa kilo ikilinganishwa na Sh 1,874 kwa kilo mismu uliyopita mwaka 2023/2024.
Aidha mapato ya mkulima yameongezeka mfano yule mwenye hakari mbili na nusu za shamba kutokana na kuogezeka kwa uzalishaji huo, mapato yake yameongeza kutoka zaidi ya Sh milioni 1 msimu wa mwaka 2023/2024 hadi kufikia zaidi ya Sh milioni 4 msimu wa mwaka 2024/2025.



