Vicoba bila usajili ni kuitafuta jela

DODOMA: Kuendesha shughuli za huduma ndogo za fedha ( VICOBA ) bila usajili kutoka Benki Kuu ya Tanzania ni kosa la jinai, adhabu yake ni faini Sh milioni 1-10, kifungo cha miaka miwili hadi mitano au vyote.
Ili kukomesha utaratibu wa kuwa na Vicoba visivyosajiliwa, BoT imetoa onyo wahusika kuacha, pia wananchi kutoa taarifa wanapoona mtu au kundi likiendesha huduma za fedha bila usajili.
Akizungumza leo Novemba 20, katika semina ya waandishi wa habari jijini Dodoma, Dickson Gama, Meneja wa Usimamizi Huduma Ndogo za Fedha BoT, amekiri kuwa huduma hizo zimekuwa na msaada kwa wananchi, lakini zinapaswa kuboreshwa usimamizi wa fedha, kutumia mifumo ya uwazi na uaminifu.

Aidha, Gama ametaja hatua zingine kuwa ni kusimamisha au kufuta usajili, au viongozi wake kusimamishwa kutoa huduma, kutoa onyo au amri kurekebisha mapungufu.
Pia ameorodhesha baadhi ya changamoto zinazojitokeza kuwa ni ukosefu wa takwimu kutoka sekta ya huduma ndogo ya fedha.
https://www.instagram.com/p/DRSWQcZjj2J/?igsh=MWN1dmV4amgwZGtnaQ==
“Kutotendewa haki wanachama, kukosekana kwa uwazi kwa viongozi wa Vicoba,” amesema Gama.
Hata hivyo, hadi kufikia Septemba mwaka huu vikundi 70,900 vimeshasajiliwa kupitia Wezesha Portal chini ya OR-TAMISEMI na kusisitiza usajili huo unatekeleza Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya 2018 inayolenga kuimarisha usimamizi wa sekta hiyo.



