Vigogo BBC kujibu tuhuma Bungeni

VIONGOZI wa ngazi ya juu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) wanaohusishwa na sakata ya hivi karibuni ya uhariri wanatarajiwa kufika mbele ya kamati ya Bunge la Uingereza Jumatatu kujibu tuhuma dhidi yao. Hatua hiyo inalenga kutoa maelezo kuhusu tuhuma za ukiukwaji wa taratibu za kitaaluma katika maandalizi na usambazaji wa taarifa za shirika hilo.

Mshauri wa zamani wa masuala ya uhariri wa BBC, Michael Prescott, ndiye atakayejitokeza hadharani kwa mara ya kwanza kutoa ushahidi kuhusu sakata hilo. Prescott ndiye aliyeibua wasiwasi kuhusu taratibu za uandaaji wa taarifa, ikiwamo marekebisho ya kipindi cha Panorama kilichohusu hotuba ya aliyekuwa Rais wa Marekani, Donald Trump.

Baadhi ya mawasiliano ya ndani aliyoyaandika yalivuja kwa vyombo vya habari na kuchangia kujiuzulu kwa Mkurugenzi Mkuu wa BBC pamoja na Mkuu wa Habari mapema mwezi huu. Wengine wanaotarajiwa kutoa ushahidi ni Mwenyekiti wa BBC, Samir Shah, ambaye anakabiliwa na shinikizo kuhusu namna alivyoshughulikia malalamiko hayo, pamoja na wajumbe wa bodi ya shirika hilo, Sir Robbie Gibb na Caroline Thomson.

Kamati ya Bunge imeeleza kuwa itajikita katika kuchunguza michakato ya Kamati ya Viwango na Miongozo ya Uhariri (EGSC) ya BBC na namna inavyosimamia uzingatiaji wa maadili ya uhariri wa shirika hilo.
Inadaiwa kuwa Prescott, aliyewahi kuwa mhariri wa siasa wa Sunday Times, pamoja na Daniel, aliyekuwa mhariri msaidizi wa Financial Times (FT), walikuwa washauri wa nje kuhusu hatari na masuala ya uhariri tangu walipoteuliwa na BBC mwaka 2022.

Wawili hao waliteuliwa kama wataalamu wa kwanza wa nje wa kusaidia EGSC katika kuhakikisha maamuzi ya uhariri yanazingatia weledi. Kikao hicho kinakuja wakati BBC ikisubiri kujua iwapo Trump ataendelea na hatua za kisheria baada ya kutishia kuifungulia mashitaka akidai fidia ya kati ya dola bilioni moja na tano kutokana na mabadiliko yaliyofanyika katika makala ya kipindi hicho cha Panorama. SOMA: Vyombo vya habari vizingatie weledi kulinda amani, uzuri wa Tanzania

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

  3. Google provides awesome remote work opportunities, allowing me to earn $2000-$3000 weekly with just 2-4 hours of daily work. It’s been a game-changer, offering flexibility and reliable income. If you’re seeking a genuine way to earn online, don’t miss this chance. Start today and transform your life!
    .
    More Details For Us →→ http://www.big.income9.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button