Vijiji vitatu Kakonko kupata majisafi na salama

KIGOMA: WANANCHI 8,984 kutoka vijiji vitatu vya Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma wanatarajia kunufaika na upatikanaji wa majisafi na salama yanayotokana na mradi wa uchimbaji visima unaosimamiwa na Wakala wa Majisafi Mijini na Vijijini (RUWASA).

Kaimu Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kakonko, Respicius Kahamba amesema hayo wakati akitoa taarifa kwa Kiongozi wa Mbio wa Mwenge wa Uhuru, Ismail Ally Ussi alipotembelea kuweka Jiwe la Msingi la mradi huo unaotekelezwa katika kijiji cha Luhuru wilayani Kakonko.

Mhandisi Kahamba amesema kuwa mradi huo unatekelezwa kwa gharama ya Sh milioni 357.3 ambapo kati ya hizo Sh milioni 355.8 zinatoka Serikali Kuu kupitia mfuko wa maji na kiasi cha Sh milioni 1.5 zinatokana na nguvu za wananchi na kwa sasa mradi umefikia asilimia 85 ukinufaisha vijiji vya Nyamtukuza, Kihomoka na Luhuru.

Mmoja wa wananchi wa kijiji,Mathias Gabriel akieleza adha walizokuwa wanazipata kutokana na changamoto ya ukosefu wa maji safi na salama ni pamoja na kutembea umbali mrefu kutafuta maji lakini pia kutumia maji ya kwenye madimbwi ambayo yalikuwa chanzo kikubwa cha magonjwa ya tumbo ikiwemo Taifod na kuhara.

Akizungumza kabla ya kuweka Jiwe la Msingi la mradi huo Kiongozi za Mwenge wa Uhuru, Ismail Alli Ussi amesema kuwa kazi kubwa imefanywa na serikali katika kupeleka huduma kwa wananchi ikiwemo kuanzishwa kwa RUWASA ili kurahisisha utekelezaji wa miradi ya maji lakini pia kuhakikisha maji safi na salama yanapatikana karibu na wananchi.

Kiongozi huyo wa Mbio za mwenge wa Uhuru mwaka huu amesema kuwa pamoja na kazi kubwa inayofanywa na serikali lakini anawashangaa watu wanaosema serikali haijafanya kitu ambapo amesema kuwa wananchi hao ni mash uhuda wa mambo mazuri yanayofanywa na serikali ya Samia Suluhu Hassan.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button