Viongozi wa dini washauriwa kuepuka uchochezi

DAR ES SALAAM: Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji wa Filamu Tanzania, Chiki Mchoma, ametoa wito mzito kwa baadhi ya viongozi wa dini kuacha kutumia majukwaa ya kidini kama uwanja wa maigizo na uchochezi unaoweza kuhatarisha amani ya taifa.
Akizungumza leo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Chiki amesema kuwa baadhi ya viongozi hao wamekuwa wakitumia maandiko matakatifu kwa namna ya kuibua taharuki na kuchochea hisia kali miongoni mwa wananchi.
Mchoma amewataka watumishi wa dini kuheshimu majukumu yao na kuacha kuingiza masuala ya kisiasa na uchochezi katika nyumba za ibada.
Aidha, amezungumzia kuhusu wanaharakati wanaojificha nyuma ya pazia la haki huku wakitaka kuvuruga utulivu wa nchi.
“Wengine wanavaa ngozi ya kondoo lakini ndani ni mbwa mwitu.kwenye biblia Meshaki, Shedracki na Abelnego walikataa kuabudu sanamu kwa utaratibu sio wanavyofanya wengine.
Kwa upande wake, mwigizaji Jimmy Mafufu ametoa amesema viongozi wanaoongea hovyo kila siku wamefika mwisho kama filamu inavyoisha.
“Sisi Tanzania hawawezi kukaa kimya wakati wachache wakijaribu kuvuruga mshikamano wa kitaifa.
Mafufu amewashauri Watanzania kuendelea kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake wa busara, akisisitiza kuwa vyombo vya usalama vinafanya kazi kikamilifu kuhakikisha taifa linasalia kuwa na utulivu.
“Ukikichafua hata sadaka unazopata utazikosa na hakuna kiongozi mzuri aombe machafuko.
“Rais wetu ni imara. Yeyote anayempinga anapingana na maslahi ya taifa. Sisi vijana tuko tayari kuilinda nchi yetu kwa hali na mali. amehitimisha.



