Viongozi wa dini watoa wito kudumisha amani

DAR ES SALAAM: VIONGOZI wa dini kutoka madhehebu mbalimbali nchini wamekutana kujadili umuhimu wa kudumisha amani, haki na maridhiano hasa wakati huu ambapo Watanzania wanajiandaa kushiriki katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29,mwaka huu.
Viongozi hao wamezungumza hayo Dar es salaam mapema wiki hii katika Kongamano la majadiliano ya kidini lililoandaliwa na kanisa la Evangelical Fellowship na kituo cha Utamaduni cha Iran kwa kushirikiana na taasisi nyingine mashuhuri za kidini na kielimu ili kujadilia masuala yanayohusu amani haki na maridhiano.
Akizungumza katika kongamano hilo Kiongozi wa Kanisa la Evangelical Fellowship Church Tanzania (EFCT), Askofu Charles Howard, Mkuu wa Kanisa hilo, alisema Tanzania inasifika kwa utulivu wa kipekee unaopaswa kulindwa.
“Huu si wakati wa kutafuta ukombozi bali mabadiliko kupitia viongozi tunaowachagua. Kama viongozi wa dini, tumekutana kujadili nafasi yetu katika kuhakikisha amani na umoja vinaendelea kudumu,” alisema Askofu Howard.
Alisisitiza kuwa Tanzania ni zawadi ya kipekee iliyopewa na Mungu kupitia Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, na Watanzania wanaposema ‘Tanzania Yetu’ ni kutokana na tunu ya amani waliyobarikiwa, hivyo aliwataka kulinda amani bila kujali utofauti wa dini au itikadi.
Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Ubalozi wa Iran nchini, Dk Mohsen Maarefi, alizungumzia umuhimu wa kuheshimu haki na usawa wa binadamu dunia na vyote vilivyomo ndani yake havina thamani kuliko damu ya binadamu.
Hivyo alisisitiza lengo la kukutana na kujadili masuala hayo ni kutokana na hatua ambayo Tanzania wanaiendea ya uchaguzi mkuu ili viongozi wa dini kuchukua nafasi yao kuhimiza kudumisha amani.
Kwa upande wake, Kiongozi wa Kanisa la Tumaini la Mataifa Yote (HOFAN), Askofu Godfrey Songambele alisema amani haiwezi kudumu bila imani thabiti kutoka kwa viongozi na wananchi. Alisema kila kiongozi wa dini ana watu wanaomtii, hivyo ni busara viongozi wa kitaifa kushirikiana nao ili kuwaunganisha Watanzania kupitia imani.
Aliongeza kuwa maandamano na migogoro mingi huzaliwa kutokana na kukosekana kwa misingi ya kiimani katika jamii, na kuwataka viongozi wa dini kujenga msingi imara wa maadili na kuhubiri umoja.
Mwanzilishi wa taasisi ya Safina-tus-salaam, Sheikh Mulaba Swalehe alieleza kuwa viongozi wa dini ni warithi wa viongozi wa kitaifa kwa sababu wana jukumu la kulea jamii kiroho na kimaadili.
Hivyo aliwasisistiza watu kufanya mchakato huo wa uchaguzi kwa utulivu na amani kwani uchaguzi ni msingi wa demokrasia na watu wakatimize haki yao ya kikatiba kuchagua wanaowaona wanafaa na si kuchochea machafuko.
Kwa upande mwingine, Mkurugenzi wa Maendeleo na Uhamasishaji Rasilimali kutoka Kanisa Katoliki, Jovin Riziki, alisema karibu asilimia 90 ya Watanzania wana imani za dini, hivyo viongozi wa dini wana nafasi kubwa ya kutoa matumaini na maadili mema kwa jamii.
“Matamko ya viongozi wa dini huchukuliwa kwa uzito mkubwa kwa sababu ya kuaminiwa na waamini wao. Wao ndio wanaokutana mara kwa mara na wananchi na kufahamu changamoto zao,” alisema Riziki.
Aliongeza kuwa umasikini huongezeka pale ambapo migogoro inachochewa, hivyo kudumisha amani ni msingi muhimu wa maendeleo endelevu.
I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com