Vituo vya afya 898 vyatoa huduma upasuaji wa dharura

DODOMA: SERIKALI imesema hadi Desemba 2025 ilikuwa imekamilisha ujenzi na ukarabati wa vituo vya afya 898, ambavyo vinatoa huduma ngazi ya kituo cha afya, ikiwa ni pamoja na huduma za upasuaji wa dharura.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi) anayeshughulikia afya, Dk Rajab Seif amesema hayo leo bungeni akijibu swali la Mbunge wa Sumve, Moses Bujaga aliyetaka kujua lini serikali itatimiza ahadi ya ujenzi wa Vituo vya Afya Walla, Mwambomba, Mwagi, Mhandi na Mwamala.

“Katika kipindi cha mwaka 2021/22 hadi 2024/25 Serikali imeendelea kuboresha miundombinu ya kutolea huduma za afya kwa ujenzi wa vituo vya afya katika kata za kimkakati kote Nchini zikiwemo Kata za Isunga, Kadashi, Kikubiji na Hungumalwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba.

“Hadi kufikia Desemba, 2025 Serikali ilikuwa imekamilisha ujenzi na ukarabati wa vituo vya afya 898 ambavyo vinatoa huduma ngazi ya kituo cha afya ikiwa ni pamoja na huduma za upasuaji wa dharura.

“Serikali itaendelea kutenga fedha za kujenga vituo vya afya katika Kata za kimkakati ikiwemo Kata ya Walla ambayo imetengewa shilingi milioni 250 katika mwaka 2025/26, utekelezaji utaendelea kwenye kata zitakazokidhi vigezo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba kadiri fedha zitakavyopatikana,” amesema.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button