Viziwi wapewa elimu utambuzi noti bandia

TANGA: MKUU wa mkoa wa Tanga, Dk Batlida Burian ameiomba Benki Kuu ya Tanzania kuendelea kuwajengea uwezo wananchi hususani wenye mahitaji maalum kuhusu utambuzi wa noti bandia .
Kauli hiyo imetolewa kwa niaba yake na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Sebastian Masanja wakati akifungua mafunzo kuhusu utambuzi wa noti bandia kwa viziwi waliopo mkoani Tanga.
Amesema kuwa iwapo kundi hilo likipata uwelewa itasaidia juhudi za serikali za kupambana na uwepo wa noti bandia na kuepuka kuingia matatizo bila ya kujua.
“Elimu hii ya utambuzi waliyoipata ikatumike kuwasaidia wengi wenye mahitaji maalum ambao ni kundi kubwa katika jamii kwani uwelewa ukiifikia jamii yote itasaidia kupunguza au kumaliza changamoto ya noti bandia,” amesema Masanja.
Kwa upande wake Ofisa Uhusiano kutoka BOT George Hela amesema kuwa elimu hiyo wamekuwa wakiitoa mara kwa mara kwenye makundi ya watu mbalimbali hapa nchini.
Amesema kuwa lengo ni kuhakikisha wanadhibiti matumizi ya hela hapa nchini hapa nchini lakini na kuongeza uwelewa kwa wananchi waliowengi.